Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4580

SOKO LA BIDHAA GHAFI KUNUFAISHA WAKULIMA

$
0
0
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), Reginald Mengi  amesema ukombozi wa upatikanaji wa masoko ya mazao ya wakulima ni uanzishwaji wa soko la bidhaa ghafi ambalo litawasaidia wakulima kujua sehemu ya kuuza mazao yao.
Akifungua mkutano  wa wadau ambao walikuwa wanaangalia nafasi ya ushiriki wao katika hilo jana, Dar es Salaam, Mengi alisema sekta binafsi inaamini kuwa mfumo huo ndio utakaosaidia ukuzaji wa masoko kwa bidhaa za wakulima na bidhaa nyinginezo ambazo zinauzwa ghafi.
"Nimeambiwa kuwa maandalizi ya kuanzishwa kwa mfumo kwa sasa uko katika hatua za juu, na sisi sekta binafsi tuna jukumu la kuhakikisha mpango huu unaanzishwa na unafanya kazi," alisema.
Soko hilo litakapoanzishwa taasisi ya sekta binafsi itakuwa inamiliki asilimia 51 huku asilimia 49 itamilikiwa na asasi na taasisi mbalimbali za serikali.
Mengi aliwataka washiriki wa mkutano kutoa mapendekezo yao ni kipi TPSF inatakiwa kufanya kwa kushirikiana na Serikali ili mpango huo uweze kuwa wenye mafanikio na kuisaidia nchi kusonga mbele kimaendeleo mara utakapoanzishwa.
Alisema sehemu ya kuanzia ili mpango huo uweze kuwa na mafanikio, ni kufanya mapinduzi kwenye kilimo, hivyo akawataka washiriki wa mkutano huo kutoa ushauri wao ili sekta hiyo ambayo imeajiri watu wengi nchini iweze kuchangia katika kupunguza umasikini hapa nchini.
Mengi alisema wakulima na kampuni kubwa wameshaonesha nia ya kuwekeza katika kilimo. Alisema wanaingia huko wakati tayari wanamiliki usindikaji, usambazaji na masoko ya sekta hiyo duniani.
Alisema hata pale taarifa zinapopatikana, kumekuwa na vikwazo vingine vya kisera pamoja na ukosefu wa fedha kufanyia biashara, jambo linalowafanya washindwe kufaidika na masoko hayo.
Wakulima na wafanyabiashara wengine watafaidika na mfumo huo kwa kuwa watakuwa na taarifa za masoko na watafahamu bidhaa gani waipeleke wapi pamoja na bei yake.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4580

Trending Articles