Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4500

VODACOM YASAIDIA KITUO CHA YATIMA SHILINGI MILIONI 10

$
0
0
Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania kupitia mfuko wake wa kusaidia jamii wa Vodacom Foundation imetoa Sh milioni 20 ili kusaidia miradi ya ushonaji na ufugaji inayotarajiwa kuanzishwa na Kituo cha Kiislamu cha Kulelea Watoto Yatima na Ushauri cha Mwandaliwa kilichopo Mbweni, Dar es Salaam.
Hundi ya fedha hizo imekabidhiwa kituoni hapo na wafanyakazi wa Vodacom waliokitembelea kituo hicho, jana.
Akikabidhi hundi hiyo, kwa niaba ya Vodacom Foundation, mmoja wa wafanyakazi wa kampuni hiyo, Angela Mwakasege alisema Vodacom kupitia mfuko wake wa kusaidia jamii wa Vodacom Foundation wakati wote inaguswa na changamoto zinazoizunguka jamii ikiwemo suala la watoto yatima na waishio kwenye mazingira magumu, ndiyo maana imejitokeza kusaidia.
Alisema hatua ya kukabidhi fedha hizo pamoja na zawadi za vitabu na vifaa mbalimbali vya kuchezea watoto ni kielelezo cha jinsi ambavyo wafanyakazi na kampuni kwa ujumla inavyoguswa na kusukumwa kusaidia jamii na kuweka mbele ajenda ya kusaidia kukabiliana na changamoto hizo
Kituo hicho chenye watoto 94 kinatarajia kuanzisha miradi ya ushonaji na ufugaji itakayotumika kukiwezesha kituo kuwa na vyanzo vya mapato na pia kuwa na fursa ya kuwajengea uwezo wa stadi za kazi na kujiajiri watoto ili kuwapa uwezo wa kujitegemea katika siku za usoni.
Akisoma maelezo ya kituo na shukrani kwa Vodacom Foundation na wafanyakazi wa Vodacom kwa kile walichowezeshwa, Katibu wa kituo hicho, Omary Ramadhan alisema watoto walio wengi hupatikana kwa kuletwa kupitia Ofisi za Ustawi wa Jamii Wilaya ya Kinondoni na husomeshwa na wengi wao wapo katika ngazi mbalimbali za elimu kuanzia ya chekechea.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4500

Trending Articles