Kesi ya kusambaza dawa feki za Ukimwi (ARVs), inayomkabili Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda cha kutengeneza dawa Tanzania Pharmaceutical Industries Ltd (TPL), Ramadhani Madabida na wenzake inatarajiwa kuanza kusikilizwa Julai 28 mwaka huu.
Wakili wa Serikali, Jackline Nyantori alidai jana mbele ya Hakimu Mkazi, Nyigulila Mwaseba wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kuwa kesi hiyo ilipotajwa.
Hakimu Mwaseba aliahirisha kesi hiyo hadi Julai 28 mwaka huu kwa ajili ya kuanza kusikiliza mashahidi wa upande wa Jamhuri.
Mbali na kushitakiwa kwa kusambaza dawa hizo, Madabida na wenzake wanadaiwa kusababisha hasara ya Sh milioni 148 baada ya kusambaza dawa hizo kupitia kiwanda chake cha Tanzania Pharmacetical kwa Bohari ya Dawa Tanzania (MSD).
Washitakiwa wengine katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi ni wafanyakazi wa kiwanda hicho Mkurugenzi Uendeshaji, Seif Shamte, Meneja Masoko, Simon Msoffe na Mhasibu Msaidizi, Fatma Shango na wafanyakazi wa MSD, Meneja Udhibiti Ubora, Sadick Materu na Ofisa Udhibiti Ubora, Evans Mwemezi.
Inadaiwa Aprili 5 mwaka 2011, Madabida, Shamte, Msoffe na Fatma walisambaza MSD makopo 12,252 ya dawa bandia za ARVs wakidai zimetengenezwa Machi 2011 na mwisho wa matumizi ni Februari mwaka jana jambo mbali sikweli.
Awali, katika maelezo ya awali (PH), Wakili Osward Tibabyekoma alidai Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) ilithibitisha kuwa dawa zilitengenezwa na kampuni hiyo ni za kughushi.