Aliyekuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, John Lubuva na wenzake wameachiwa huru baada ya upande wa Jamhuri kushindwa kuthibitisha kesi iliyokuwa ikiwakabili ya kutumia vibaya madaraka, kula njama na kuitia serikali hasara ya Sh bilioni 1.7.
Kesi hiyo ilifunguliwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mbele ya Hakimu Mwandamizi, Hassan Juma.
Juma alisema Jamhuri imeshindwa kuthibitisha ni jinsi gani ubomoaji wa nyumba zilizokuwa maeneo ya Tabata Dampo ulikuwa ni kinyume na sheria.
Alisema katika mashitaka hayo kulikuwa na uamuzi wa Mahakama ya Ardhi na Baraza la Nyumba lililowataka wahame kwa kuwa walikutwa na hatia hivyo waliamriwa wahame kwani hawakuwa na hati za makazi hayo.
Pia alisema haikuwa na ulazima kwa kuwapa wakazi hao barua za kuwataarifu kuwa wanatakiwa kuhama kwani wanajua ni kosa.
Hakimu Juma alisema watu 88 pekee walipewa fidia ya Sh milioni 20 wakati kila nyumba ilikuwa na thamani tofauti na ilivyoelezwa awali katika mashitaka hayo.
Aliongeza kuwa ni waathirika 71 pekee ambao walipata madhara katika bomoa bomoa hiyo.
Aidha, kwa upande wa mashahidi hakuna muathirika yeyote aliyetoa ushahidi juu ya mashitaka hayo hivyo kushindwa kuthibitisha kama washitakiwa hao walitumia vibaya madaraka na kuwaathiri watumiaji wa kiwanja hicho.
Pia Jamhuri ilishindwa kuthibitisha kuwa Lubuva na wenzake kama walikula njama ili kufanya makosa hayo.
Kwa mara ya kwanza Lubuva, Mhandisi wa Manispaa ya Ilala Idd Kisisa, Mkuu wa Idara ya Sheria na Ulinzi, Anderson Msumbi na Mwanasheria Andrew Kanonyele walifikishwa mahakamani hapo Julai 2011 kwa tuhuma za kula njama na kutenda kosa la kuvunja makazi ya watu katika kiwanja namba 52 kilichopo Barabara ya Mandela,Tabata jijini Dar es Salaam.
Walidaiwa Februari 28,2008 kuwa na mashitaka matatu ya kuisababishia Serikali hasara hiyo ya kula njama na kutumia vibaya madaraka.