Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4503

JWTZ KUJENGA DARAJA MABWEPANDE

$
0
0
Manispaa ya Kinondoni imeingia makubaliano na Shirika la Mzinga Holdings la Jeshi la Wananchi (JWTZ) mkoani Morogoro kwa ajili ya ujenzi wa daraja katika eneo korofi la Mabwepande.
Makubaliano hayo yamefanyika jana jijini Dar es Salaam mbele ya wananchi wa eneo hilo na Meya wa Manispaa hiyo, Yusuph Mwenda na Meneja Mkuu wa shirika hilo, Meja Jenerali Charles Muzanila. Awali, akizungumza kabla ya kutia saini makubaliano ya ujenzi wa daraja hilo, utakaogharimu Sh milioni 301, Diwani wa Kata ya Mabwepande, Clement Boko alisema  eneo hilo limekuwa ni kero kubwa kwa wakazi hao,  hasa mvua zinaponyesha kwani mawasiliano yanakatika. 
Alisema tatizo hilo ni la muda mrefu, hasa kwa  wakazi hao, hasa wa Mtaa wa Kikwete Visheni, hali iliyofanya apigie kelele suala hilo kwenye Baraza la Madiwani.
Mwenda aliwathibitishia wananchi hao, kuwa kero hiyo imefika mwisho,  kwani ujenzi huo utakamilika baada ya miezi mitatu. Alisema daraja hilo litakuwa ni kubwa.
Aliwataka wananchi hao, kutoishia kulalamika, kama wataona mkandarasi huyo anajenga daraja hilo chini ya kiwango, bali watoe taarifa ili hatua ziweze kuchukuliwa. 
Alisema anaamini mkandarasi aliyepewa tenda hiyo ni mzuri, kutokana na kuwa mzalendo na shirika la umma hivyo hawezi kwenda kinyume.
Kwa upande wake, Meja Jenerali Muzanila alisema, hakuna shaka kuwa kazi hiyo wataitekeleza kwa wakati hasa kwa kuzingatia wanatumia vifaa na teknolojia ya kisasa waliyonayo.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4503

Trending Articles