Familia zaidi 65 hazina mahali pa kuishi katika kijiji cha Kabondo kata ya Mwanase wilayani Kahama mkoani Shinyanga.
Hali hiyo inatokana na nyumba zao kusombwa na mvua ya mawe, iliyoambatana na upepo mkali.
Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Kabondo, Elias Paul, alisema mvua hiyo ilianza kunyesha saa 8 usiku na kuzoa mazao yaliyolimwa.
Hali hiyo imesababisha wakazi wa kijiji hicho, kuhitaji msaada wa haraka ili kuokoa maisha yao.
Mvua hiyo imesababisha mpunga kwenda na maji, hali itakayosababisha upungufu mkubwa chakula katika kata hiyo.
Wananchi ambao nyumba zao zimechukuliwa na maji, kwa sasa wamehifadhiwa na majirani zao huku wakisubiri msaada kutoka katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kahama.
"Kwa sasa waathirika hao katika sehemu walizojishikiza, wanaishi zaidi ya watu 14 huku wengine wakiwa katika majiko ya kupikia, hali ambayo inaweza kusababisha kufumuka kwa magonjwa ya kuambukiza kama vile kipindupindu", aliongeza ofisa Mtendaji huyo wa Kijiji cha Kabondo.