Vikosi vya Zimamoto vya Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jana vilikuwa na kazi ya kuondoa maji yaliyotokana na mvua yalioyokuwapo uwanjani hapo.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Fadhili Manongi jana alipotakiwa kutoa taarifa za uwanja wa ndege kufuatia mvua kubwa zilizonyesha mwishoni mwa wiki.
"Hali ya uwanja wa ndege uko vizuri na kwa sasa vikosi vya zimamoto vinaondoa maji yaliopo uwanjani hapo. Na tunashukuru Mungu kuwa leo (jana) jua limewaka kidogo," alisema.
Aidha, Manongi alisema shughuli za ndege kutua na kuruka zilikuwa zikiendelea kama kawaida kutokana na njia za kuruka na kutua ndege kutoathirika na maji ya mvua.
"Mpaka sasa hatujifikiria kufunga uwanja kwasababu hali ya uwanja sio mbaya na shughuli zimekuwa zikiendelea kama kawaida," alisema.