Mwanamuziki nguli wa muziki wa dansi nchini, Maalim Muhidin Gurumo amefariki dunia leo mchana kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam alikokuwa amelazwa kwa matibabu.
Gurumo ambaye alikuwa kiongozi wa muda mrefu wa bendi ya Msondo Ngoma Music Band kabla ya kutangaza kustaafu mwaka jana, alifikwa na umauti baada ya kusumbuliwa na maradhi kwa kipindi kirefu, hali iliyomsababishia kufikia uamuzi wa kustaafu muziki.
Mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwa marehemu Mabibo Makuburi ambapo ndiko kwenye msiba.
Mungu ailaze roho ya marehemu Gurumo mahali pema peponi, Amina.