Hatimaye baada ya miaka kadhaa ya kuishia kushika nafasi ya pili, timu ya soka ya Azam imetawazwa rasmi kuwa mabingwa wapya wa Ligi Kuu ya Vodacom baada ya kuichapa Mbeya City mabao 2-1 katika mchezo mkali uliomalizika muda mfupi uliopita kwenye Uwanja wa Sokoine, jijini Mbeya.