![]() |
Shekhe Ponda Issa Ponda (wa tatu kutoka kulia) akiwa mahakamani na wenzake kusikiliza kesi dhidi yao. |
Katibu wa Taasisi na Jumuiya za Kiislamu, Shehe Ponda Issa Ponda na wafuasi wake 49, wamekutwa na kesi ya kujibu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam.
Shehe Ponda na wenzake wanakabiliwa na mashitaka ya uchochezi na wizi wa mali zenye thamani ya Sh milioni 59.
Hakimu Victoria Nongwa alitoa uamuzi huo jana, baada ya kupitia majumuisho ya hoja yaliyowasilishwa mwishoni mwa wiki iliyopita na mawakili wa pande zote, kama washitakiwa wana kesi ya kujibu au la.
Shehe Ponda anatarajiwa kupanda kizimbani kesho, kuanza kutoa utetezi wake, kwa kuwa ndiye mshitakiwa wa kwanza katika kesi hiyo.
Akisoma uamuzi huo, Hakimu Nongwa alisema upande wa mashitaka umejenga kesi dhidi ya washitakiwa, kutokana na ushahidi wa mashahidi 17 na vielelezo vilivyowasilishwa mahakamani hapo, hivyo washitakiwa wanatakiwa kuanza kujitetea.
Alisema baada ya kupitia hoja hizo, aliona ni vema washitakiwa wapande kizimbani kujitetea na kuieleza Mahakama walikuwa wanafanya nini usiku wa Oktoba 16 mwaka jana, katika kiwanja cha Chang’ombe Markazi ambako walikamatwa.
Alisema kutokana na ushahidi uliotolewa, chanzo cha kesi hiyo ni kiwanja cha ekari nne kilicho eneo la Chang’ombe Markazi, ambacho Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), walibadilishana na Kampuni ya Agritanza kwa ekari 40 zilizo Kisarawe mkoani Pwani.
Hakimu Nongwa alisema Bakwata walipobadilishana kiwanja hicho na Kampuni ya Agritanza, Waislamu hawakufurahishwa wala kuridhika na mabadiliko hayo.
Kutokana na kutoridhishwa huko, alisema ndipo Waislamu hao walipokwenda kukomboa kiwanja chao, wakiamini atakayedai kiwanja chake, ndiye atakayekwenda mahakamani.
“Nafananisha mgogoro huu na baba aliyeamua kuuza nyumba, halafu watoto wake wasiridhike na uamuzi huo. Lakini wanachotakiwa ni kupeleka malalamiko yao mahakamani na si vinginevyo,” alisema.
Hakimu Nongwa alisema ushahidi upo wazi, kuwa walibadilishana ardhi, lakini kwa kuwa suala hilo limetokana na mgogoro wa ardhi, hamzuii mtu ambaye hataridhika kwenda kufungua shauri hilo katika Mahakama ya Ardhi ambayo itatoa uamuzi zaidi.
Washitakiwa wanakabiliwa na mashitaka matano, ambayo ni kula njama ya kutenda kosa, kuingia kwa nguvu katika kiwanja hicho Chang’ombe Markazi, kwa nia ya kutenda kosa Oktoba 12 mwaka jana.
Inadaiwa pasipo uhalali, washitakiwa walitenda kosa la jinai kwenye kiwanja kinachomilikiwa na Kampuni ya Agritanza na kujimilikisha kiwanja hicho kwa njia iliyosababisha uvunjifu wa amani.
Pia wanadaiwa kusababisha wizi wa vifaa na malighafi zikiwamo; nondo na kokoto zenye thamani ya Sh 59, mali ya kampuni hiyo.
Katika mashitaka ya uchochezi, ambayo yanawakabili Shekhe Ponda na Swaleh Mukadam, wanadaiwa Oktoba 12 katika eneo hilo, walihamasisha washitakiwa hao watende kosa hilo.
Shekhe Ponda na Mukadam wanaendelea kusota rumande baada ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), kuzuia dhamana yao huku washitakiwa wengine wakiwa nje kwa dhamana.