Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4621

NHC YAWEKA SOKONI NYUMBA ZAKE 118 ZA MAKAZI...

$
0
0
David Shambwe.
Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kwa mara nyingine jana limezindua mradi mpya wa mauzo ya nyumba za makazi ya familia 118 katika Mtaa wa Wakulima, Hananasif, wilayani Kinondoni.
Nyumba hizo zinagharimu kati ya Sh milioni 199 hadi Sh milioni 253.
Aidha, mauzo ya nyumba hizo zinazojengwa kwa mtindo wa ghorofa, yanaanza Aprili 23 mwaka huu.
Shirika hilo limetoa angalizo kwa wanunuzi, kuepuka utapeli unaofanywa na baadhi ya watu kujiita madalali wa shirika hilo na kusisitiza hakuna udalali kwa mauzo ya nyumba zao.
Mkurugenzi wa Uendeshaji Biashara, David Shambwe aliwaambia waandishi wa habari jana, Dar es Salaam kuwa, nyumba hizo zina vyumba vitatu vya kulala, kimoja kikijitegemea kwa maliwato (master bedroom) na kwamba makazi hayo yamewekewa eneo la kuogelea, mgahawa na sehemu ya mazoezi.
“Mradi huu upo kilometa sita kutoka katikati ya Jiji na ikifika Aprili 23 tutaanza kupokea fedha, kwa watakaolipa fedha yote katika siku 90 kutakuwa na punguzo maalum la asilimia sita ambalo ni wastani wa Sh milioni 10,” alisema Shambwe na kueleza kuwa hadi mradi huo ukamilike utagharimu Sh bilioni 20.
Kwa upande wake, Mhandisi wa Mradi kutoka Kampuni ya Estim Construction Co Ltd, Anna Mrema, akizungumza na waandishi katika eneo la mradi, alisema ujenzi wa makazi hayo utakamilika Aprili mwakani na unahusisha ghorofa 15 na eneo la kutosha la kuegesha magari.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4621

Trending Articles