Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4550

MKUU WA MKOA CHUPUCHUPU MTEGO WA SIKU YA WAJINGA...

$
0
0
Dk Rajab Rutengwe.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi , Dk Rajab Rutengwe  ametoa ushuhuda wake  jinsi  alivyoponea chupuchupu,  kuhadaiwa  na mkazi mmoja  mjini Mpanda jana asubuhi,  ambayo ilikuwa Siku ya Wajinga Duniani.
Dk Rutengwe  alitoa  ushuhuda  wake  mbele  wa  wadau  wa  kikao,  kilichowakutanisha  kujadili  sheria  ndogo  za uanzishwaji wa  Mfuko  wa Bima ya Afya (CHF) na Tiba  kwa Kadi (TIKA) kilichofanyika  leo  mjini hapa.
wadau  wa  kikao  kilichokutanisha  kujadili  sheria  ndogo  za uanzishwaji wa  Mfuko  wa Bima ya Afya (CHF) na Tiba  kwa Kadi (TIKA) kilichofanyika  leo  mjini hapa.
“Leo (jana) asubuhi  nusura niingizwe  mjini,  kwani  nilikuwa  sina  habari kuwa  ni  Siku ya Wajinga Duniani, nilipokea  simu  ya  mtu mmoja  ambaye  hakujitaja jina,  akaniomba msaada  eti  alikuwa  ameunguliwa na  nyumba yake  na  kupata hasara kubwa  ya vitu  vyake  vya  thamani  kuteketea kwa  moto,” alisema.
Aliendelea kusema, “lakini  baada ya  kufikiria  kwa kina  na kujiuliza mbona  Kamati  ya Ulinzi  na Usalama ya Mkoa  pia  ya Wilaya  hazijanipa ripoti,  ndipo  baadaye  nikabaini  kuwa  leo (jana)  ilikuwa  ni Siku ya Wajinga Duniani.”
Awali,  akimkaribisha mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaya  ya Mpanda, Paza Mwamlima  aliguswa  na mahudhurio  makubwa  ya  wakuu wa idara.
“ Nimeguswa  sana  na mahudhurio  makubwa,  hususani  ya  watendaji  wenu, ambao mara  nyingi  hawahudhurii  vikao  vyetu,  ambavyo  havina posho  sasa  baada ya kusikia  kuwa  kikao  hiki  inatolewa  posho    wamehudhuria  kwa wingi,” alisema Mwamlima.
 Kaimu Mkurugenzi  Mkuu  wa Bima ya  Taifa ya Afya (NHIF), Celestine Mugongo  alisema  halmashauri  zipatazo   40 katika mikoa mbalimbali  nchini, zitaunganishwa katika mpango wa huduma ya Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF), ikiwa ni mkakati wa NHIF kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma bora za matibabu.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4550

Trending Articles