Hatimaye mvutano kuhusu kura gani itumike, kati ya wazi na siri kufanya uamuzi katika Bunge Maalumu la Katiba, umefikia tamati baada ya Kamati ya Kanuni na Haki za Bunge Maalumu, kuamua kura zote zitumike kufanya uamuzi mmoja.
Hata hivyo, wakati uamuzi huo ukionekana kuwa wa maridhiano, kwa kuwa kila mjumbe atakuwa huru kuamua kura atakayoipiga, bado kama ilivyotarajiwa, baadhi ya wajumbe hasa kutoka kundi la Umoja wa Katiba ya Wananchi, wameelezea kutoridhika.
Jana Mwenyekiti wa Kamati ya Kanuni na Haki za Bunge Maalumu, Pandu Ameir Kificho, aliwasilisha mapendekezo ya Azimio la Bunge Maalumu, la kufanya marekebisho ya Kanuni ya 37 na 38, ili Bunge liazimie kura zote zitumike.
“Kanuni zetu za Bunge Maalumu zimeweka fursa hiyo ya kufanya marekebisho au mabadiliko ya kanuni hizo.
Dhamira ya kufanya marekebisho haya ya kanuni inatokana na sababu ifuatayo.
“Jambo la msingi lililosababisha kufanya mabadiliko ya kura zetu, ni msingi wa kanuni ya 38 (2) ya Kanuni za Bunge Maalumu ambayo ilieleza kuwa, utaratibu wa kupiga kura utakubaliwa na Bunge hili baadaye.
“Kwa msingi huo, mabadiliko ya kanuni hizo, yanapendekeza kuziba pengo lililokuwepo katika utaratibu wa kupiga kura kwa kupendekeza kuziba pengo lililokuwepo katika utaratibu wa njia zote mbili za kura, yaani utaratibu wa kura ya siri au kura ya wazi kadri kila mjumbe atakavyochagua utaratibu wa kutumia katika upigaji kura,” alisema kificho.
Pamoja na mapendekezo hayo, mgawanyiko uliozoeleka ndani ya Bunge, kati ya Ukawa, kundi la 201 na wajumbe ambao wanatoka ndani ya CCM, waliendelea kulumbana kila mmoja akivutia kwake.
Mmoja wa wajumbe, Paul Makonda, aliweka wazi kuwa yeye ni muumini wa kura ya wazi, na anaridhika na uamuzi wa Kamati lakini akapendekeza ikiwezekana zitumike kura za elektroniki.
Hata hivyo, mjumbe kutoka kundi la 201, Pamela Masay, ambaye alisema ni mhandisi anajua kura za elektroniki zilivyo mbaya kwa kuwa zinaweza kuwekewa mfumo, kura tatu zikisema ndio, moja iseme hapana.
Alisisitiza ipigwe kura ya siri na kupinga pendekezo au jaribio lolote la kutaka kupiga kura za elektroniki.
Kura ya wazi Waliotetea kura ya wazi, wote wameunga mkono mapendekezo ya Kamati ya Kanuni na Haki za Bunge Maalumu, na wamekubali pia wanaotaka kupiga kura ya siri bila kuwapinga.
Miongoni mwao ni pamoja na Mohamed Aboud, Mohamed Raza na wengine ambao karibu wote wanatoka CCM, huku hoja kubwa kwao ikiwa kura ya wazi ni ujasiri, inaonesha mjumbe yuko huru, ni hoja mpya ambayo imeonesha dunia namna Watanzania wanavyoweza kufikia maridhiano.
Waliosimamia upande wa kura ya siri, waliendelea kupinga kura ya wazi isipokuwa Ester Bulaya ambaye alitetea kura ya siri na kuunga mkono wanaotaka kura ya wazi wafuate mfumo wanaotaka.
Miongoni mwa waliozungumza ni John Mnyika, Rukia Kassim Ahmed, Masay, Ezekiel Olouch ambao hoja yao kuu ni kutaka demokrasia ilindwe ambayo imekuwa ikisisitiza kura ya siri.
Pia wamekuwa wakitetea kuwa inamfanya mjumbe kuwa huru kuamua na pia itasaidia wasidhurike kama watapiga kura ya wazi kinyume na baadhi ya watu katika maeneo wanakoishi au katika vyama vilivyowaamini.