![]() |
Rais Jakaya Kikwete wakati akizindua Bunge la Katiba jana. |
Akihutubia jana Bunge Maalumu la Katiba, Kikwete alisema jambo hilo ni jema lakini wajumbe hao wanatakiwa walitafakari kwani wale watakaoshindwa wanaweza kuleta msuguano ili mradi aliyeshinda aondolewe na wananchi.
"Kumwondoa mbunge ni jambo jema, lakini athari zake ni kubwa kwani naona kuna hatari ya kutengeneza msuguano mkubwa kwenye majimbo," alisema Rais Kikwete.
Alisema kuna hatari kwamba uchaguzi ukimalizika tu, mshindani ambaye alishindwa kwenye kura za maoni anaanza kuleta msuguano ili wananchi wamkatae mbunge wao.
Pia alipinga kitendo cha wabunge kuwekewa kikomo kwa maelezo kuwa duniani kote wanaowekewa kikomo ni viongozi wakuu na sio wabunge.
"Viongozi wakuu kuna haki ya kuwawekea kikomo ili wasigeuze nchi kama nyumba yao, lakini kwa wabunge hakuna kikomo," alisema Rais Kikwete.
Alisema ubunge pia ni njia ya kuwapika viongozi ambao wanakaa bungeni kwa muda mrefu na baadaye wanakuja kuwa viongozi wa nchi ambao wanaweza kuliongoza taifa vizuri kwa kuwa wanakuwa na uzoefu wa kuongoza siasa.
Eneo lingine ambalo Rais alilipinga ambalo limeainishwa kwenye rasimu hiyo ni wananchi kumwondoa mbunge wao anayekuwa ameumwa mfululizo kwa kipindi cha miezi sita jambo ambalo alisema ni ukatili kwa mbunge husika.
Alisema ni vyema mbunge aondolewe pale anapowekwa kizuizini kwa muda wa miezi sita na sio kumwondoa kwa ugonjwa, hivyo akawataka wajumbe wa Bunge hilo kuliona hilo wanapoenda kuandika Katiba mpya.