![]() |
Moja ya maiti hizo ikipakwa vipodozi. |
![]() |
Moja ya maiti ikitembezwa mitaani huku ikiwa imevalishwa suti ya gharama. |
Kila mwili katika eneo hilo hufukuliwa na kufanyiwa sherehe kila baada ya miaka mitatu.
Hayo yalidhihirika hivi karibuni baada ya familia moja kufukua maiti ya mama yao, kuivalisha nguo mpya, tena za thamani na kuichana nywele.
Haikuishia hapo, bali wakazi wengi walikusanyika na kumfanyia sherehe kubwa maiti hiyo kabla ya kuanza msafara wa kumtembeza katika mitaa mbalimbali na baadaye kuurejesha mwili kaburini alikokuwa amezikwa.
Kwa mujibu wa wenyeji wa eneo hilo, wanafanya hivyo wakiamini wafu nao wana haki ya kuendelea kuishi na kujumuika na ndugu zao waliobaki duniani.
“Ni utamaduni wa kawaida hapa kwetu. Ni fursa, heshima na njia ya kutafuta baraka kwa kumtendea haki aliyekufa. Si uungwana kumsahau kabisa mtu aliyekufa,” anasema mmoja wa wazee wa eneo hilo anayesema ameshuhudia utamaduni huo tangu miaka ya 1950.
Katika kufanikisha jambo hilo linalowaacha wengi midomo wazi, wakazi hao wanaamini kuwa, kwa kufanya wanaonesha heshima kwa maiti na kumuenzi mtu aliyekufa kwa kumwonesha upendo wa dhati.
Aidha, wakati wanapourudisha mwili kaburini, huufunga kitambaa maalumu wakiamini kuwa, kwa kufanya hivyo huzuia mwili wa marehemu kuoza.
Kwa wakazi wa eneo hili, msiba ni kitu kikubwa mno kwao. Ndiyo maana katika kipindi chote cha msiba, watu hunywa, kula na kucheza na wengine wakifunga ikiwa ni njia ya kumwombea marehemu.
Na kwa kuwa huwa shughuli kubwa, wafiwa mara nyingi miili ya marehemu haizikwa haraka.
Hufanywa hivyo ili kuwapa wafiwa muda wa kukusanya fedha za shughuli, hivyo katika kipindi chote kinachoweza kufikia hata mwaka kabla ya kuuzika rasmi mwili, maiti huwa imehifadhiwa ndani na kuwekewa dawa kuzuia isioze.
“Huangaliwa mithili ya mgonjwa na kumsemesha marehemu. Familia ikishakamilisha taratibu ndipo maziko rasmi hufanyika ama kaburini, kwenye pango au kuning’inizwa juu ya jabali,” anasema mmoja wa wazee katika mji wa Toraja.