Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemhukumu kifungo cha miaka 20 jela raia wa China, Yu Bo baada ya kupatikana na hati ya kukutwa na pembe za ndovu, zenye thamani ya Sh milioni 978.
Hakimu Mkazi Devotha Kisoka alitoa hukumu hiyo baada ya mshitakiwa huyo, kukiri kosa pamoja na maelezo ya awali yaliyosomwa na upande wa Jamhuri.
Baada ya kukiri mashitaka hayo, Hakimu Kisoka alimhukumu kutumikia kifungo cha miaka 20 jela au kulipa faini ya Sh bilioni tisa. Hata hivyo, mshitakiwa huyo alishindwa kulipa faini hiyo.
Awali, Wakili Mwandamizi wa Serikali, Faraja Nchimbi alidai kuwa Desemba 30 mwaka jana, Bo alikutwa akiwa na nyara za serikali, ambazo ni pembe za ndovu 81 zenye uzito wa kilo 303 na vipande viwili vya Kakakuona, vyenye thamani ya Sh milioni 978 bila kuwa na kibali cha Mkurugenzi wa Wanyama pori.
Alidai kuwa Bo alikamatwa akiwa na nyara hizo, zikiwa kwenye gari aina ya Mazda yenye namba za usajili T 213 BUY, katika Bandari ya Dar es Salaam wakati akitaka kuzisafirisha kwenda China.