Watu watano wamejeruhiwa vibaya na kukimbizwa katika hospitali ya wilaya ya Mkuranga, mkoani Pwani baada ya basi dogo la abiria aina ya Toyota Hiace kugongwa na lori eneo la Mwandege, Mkuranga. Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa Usalama Barabarani wa mkoa huo, Edward Mutairuka, chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa lori ambaye alihama njia na kulifuata basi hilo lililokuwa likitokea Mbagala kwenda Mkuranga.