![]() |
Gabriel Fuime. |
Alifikishwa mahakamani hapo jana na kusomewa mashitaka manne na Wakili wa Serikali Benard Kongola mbele ya Hakimu Mkazi Augustina Mmbando.
Wakili Kongola alidai kuwa Machi 29 mwaka jana katika Mtaa wa Indira Gandhi, Ilala Dar es Salaam, kwa makusudi mshitakiwa aliwaua watu wanne.
Ilidaiwa kuwa mshitakiwa aliwaua Gabriel Kamwela, Philipo Kusimala, Bethod Mwanengule na Zahda Kanji.
Mshitakiwa hakutakiwa kujibu mashitaka na kurudishwa rumande kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo isipokuwa Mahakama Kuu. Upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na kesi imeahirishwa hadi Machi 5 mwaka huu.
Kesi hiyo imefunguliwa katika mahakama hiyo kwa hatua za awali na upelelezi ukikamilika itahamishiwa katika Mahakama Kuu kwa ajili ya kusikilizwa.
Katika hatua nyingine, Madachi Hassan na Masoud Awadhi wamefikishwa katika mahakama hiyo kwa tuhuma za wizi wa nyaya za umeme za Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), zenye thamani ya Sh milioni 5.8.
Katika mashitaka mengine, Hellen alidai washitakiwa hao wakiwa kama walinzi walishindwa kuzuia uhalifu usifanyike kituoni hapo.
Mbele ya Hakimu Mkazi, Aloyce Katemana, Wakili wa Serikali, Hellen Moshi, alidai Agosti 24, mwaka jana, katika kituo kidogo cha TANESCO Mivinjeni, washitakiwa waliiba meta 64 za waya wa shirika hilo wenye thamani hiyo.
Washitakiwa walikana mashitaka na kurudishwa rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ya kuwa na wadhamini wawili wa kuaminika ambao watatia saini ya hati ya dhamana ya Sh milioni sita. Kesi itatajwa Machi 7, mwaka huu.