![]() |
Said Bwanamdogo. |
Spika wa Bunge, Anne Makinda, alitangaza msiba huo jana katika taarifa iliyotolewa na Ofisi yake na kwa kushirikiana na familia.
"Spika wa Bunge Anne Makinda anasikitika kutangaza kifo cha Mbunge wa Chalinze, Saidi Bwanamdogo, kilichotokea saa 12.30 asubuhi ya leo (jana) Moi alikokuwa amelazwa kwa matibabu," ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.
Bwanamdogo alizaliwa Desemba 24, 1968 mkoani Pwani. Kabla ya kugombea ubunge Chalinze kwa tiketi ya CCM mwaka 2010, alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Kondoa.