![]() |
William Lukuvi. |
Muswada wa Sheria ya Kura ya Maoni wa Mwaka 2013, uliowasilishwa rasmi bungeni jana unaweka masharti ya kutambua makundi ya watu, vyama na asasi za kiraia yanayokusudia kupinga Katiba hiyo.
Akiwasilisha Muswada huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, William Lukuvi, alisema kifungu cha tatu kimeweka masharti kuhusu uanzishwaji wa kamati za kura ya maoni kwa kila jimbo, ambazo zitaundwa na makundi ya watu, vyama na asasi za kiraia zinazokusudia kuunga mkono au kupinga Katiba mpya.
Sehemu hiyo pia inaweka masharti ya usajili wa kamati hizo, utakaofanywa na Tume ya Uchaguzi Tanzania (NEC) na ya Zanzibar (ZEC).
Pia kutakuwa na daftari la mawakala watakaoteuliwa na kamati hizo kusimamia kura, kampeni na gharama za kampeni.
Lukuvi alisema masharti hayo yanalenga kuweka mfumo wa uwazi kwa utendaji kazi wa kamati hizo na kutoa elimu kwa wananchi kuhusu suala linalohitaji kuthibitishwa.
Alisema upigaji kura ya maoni ili kupata Katiba mpya, utajumuisha maswali, likiwamo la wapiga kura kutakiwa kujibu ndiyo kama wanakubali Katiba mpya au hapana, kama wanaikataa.
“Utaratibu huu unatumika Tanzania Bara kwa mara ya kwanza, na utawezesha Watanzania kupigia kura suala lenye maslahi ya Taifa baada ya kuandaa swali au maswali yanayohusu kupata uamuzi wa wananchi wakati wa kupiga kura,” alisema Lukuvi.
Pia Muswada huo wenye sehemu tano, umebainisha wazi kuwa wakati wa kupiga kura ya maoni, NEC na ZEC zitatumika kusimamia.
Sehemu ya kwanza inahusu jina la Muswada, ambalo ni Sheria ya Kura ya Maoni na ukomo wake utafikiwa baada ya Katiba mpya kupatikana.
Sehemu ya pili ya Muswada, imeweka masharti kuhusu uendeshaji wa kura ya maoni na kupendekeza Rais kwa kushauriana na Rais wa Zanzibar, kuelekeza Tume kuendesha kura ya maoni kuhusu Katiba inayopendekezwa.
“Swali la kura ya maoni litaandaliwa na NEC na ZEC na litahitaji jibu la ndiyo au hapana, tofauti na utaratibu wa uchaguzi uliozoeleka wa kupigia mtu au chama kura,” alisisitiza.
Sehemu hiyo pia, inapendekeza NEC na ZEC zipewe wajibu wa kusimamia uendeshaji wa kura hiyo ya maoni na kusimamia elimu ya wapiga kura ya maoni.
Pia imeweka masharti yanayohusu uteuzi wa wasimamizi wa kura ya maoni wa kila jimbo, kusimamia upigaji kura ambapo kila msimamizi kwa kushirikiana na tume hizo, atateua maofisa na naibu maofisa wa kura ya maoni kusimamia vituo vya kura.
Lukuvi pia alisema kwa mujibu wa Muswada, mpiga kura aliyesajiliwa katika Daftari la Kudumu la Wapiga kura la NEC na ZEC, ndiye atakayekuwa na haki ya kupiga kura hiyo.
“Muswada unapendekeza walioandikishwa kupiga kura na taarifa zao zipo kwenye madaftari ya tume hizo ila wamepoteza vitambulisho vya kupigia kura, wajaze fomu maalumu na kuruhusiwa kupiga kura,” alisema.
Lengo kwa mujibu wa Lukuvi, ni kuhakikisha kila mwananchi mwenye sifa na aliyeandikishwa kwenye madaftari hayo, anashiriki kupiga kura ya maoni na tayari mchakato wa kuboresha madaftari hayo kwa Zanzibar upo katika hatua ya mwisho huku Tanzania Bara ukianza Januari mwakani.
Kuhusu sehemu ya nne ya Muswada, Lukuvi alisema kuna utaratibu wa kupiga kura ambao kimsingi hautofautiani na wa kupiga kura za uchaguzi kwa sasa, vifaa vya kupigia kura, utaratibu wa kupiga kura na utulivu katika kupiga kura.
Alisema pia sehemu hiyo imeweka masharti katika maeneo ya utaratibu wa kuahirisha au kusimamisha upigaji kura ukitokea umuhimu wa kufanya hivyo, mawasiliano na wapiga kura katika kituo cha kupiga kura na utaratibu wa kufunga masanduku ya kura.
Maeneo mengine yaliyowekwa masharti katika sehemu hiyo ya Muswada ni karatasi za kura, utaratibu wa kupiga kura, kurudia kuhesabu kura, wapiga kura wanaohitaji msaada na kutangazwa na kuchapishwa matokeo.
Kuhusu sehemu ya tano, alisema Muswada unaelezea utaratibu wa kuendesha kura ya maoni, upigaji kura katika mazingira maalumu, kuthibitishwa kwa waangalizi, mahudhurio ya mawakala, uamuzi wa malalamiko, rufaa, zuio la kuchochea vurugu na adhabu.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Katiba, Sheria na Utawala, Pindi Chana wakati akiwasilisha maoni ya Kamati hiyo kuhusu Muswada huo, alisema Kamati inapendekeza kura zitangazwe ndani ya saa 72 tangu kufungwa kwa vituo vya kupigia kura.
Alisema pia inapendekeza matokeo ya uchaguzi, yaamuliwe kwa kigezo cha asilimia 50 ya kura halali zilizopigwa za kuunga mkono swali kwa kuwa Muswada umeweka masharti kuwa wingi wa kura halali ndio utakaoamua kuhusu kukubalika au kutokubalika kwa Katiba.
Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni, Tundu Lissu na kuonesha kuridhishwa na Muswada huo lakini alipendekeza mchakato wa kutungwa kwake ufutwe, kwa kuwa uko kinyume na Katiba.
“Pamoja na mapendekezo ya maana tuliyoyaona hapa, na umuhimu wa Muswada huu kupendekeza utaratibu wa kuhalalisha Katiba mpya kwa ajili ya nchi yetu, ukweli ni kwamba ni muhimu kuzingatia Katiba iliyopo sasa,” alisema Lissu.
Alisema Katiba ya sasa haina kipengee chochote kinachozungumzia kura ya maoni na kilichotumika kama msingi wa kutungwa kwa sheria hiyo si halali.
“Endapo Muswada huu utapitishwa kuwa sheria, utakuwa umekiuka masharti ya Katiba ya sasa, na hivyo kuwa batili na kutenguka, ni muhimu kwa Bunge kutumia mamlaka yake kikatiba, kufanya marekebisho katika Katiba ya sasa na kuweka masharti yatakayoruhusu kura ya maoni,” alisisitiza.