Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4605

MCHIMBA MAKABURI ATIMULIWA KAZI KWA KUPIGA SALUTI NDANI YA KABURI...

$
0
0
Hii ndio picha iliyomponza Ray Loxton.
Mchimba makaburi amefukuzwa kazi hiyo aliyoifanya kwa miaka 40 baada ya picha yake aliyoonekana akiwa amesimama nusu uchi kwenye eneo la makaburi kuonekana ya kuchukiza na kuibua makelele miongoni mwa wasomaji wa magazeti wa mjini humo.
Ray Loxton, miaka 59, alipigwa picha katika gazeti moja la mjini humo akitabasamu, huku akiwa amesimama bila shati ndani ya kaburi wakati wa siku ya joto kali.
Pia alikuwa amejikinga macho yake na jua kwa kutumia mkono - ambao baadhi ya wasomaji wa Jarida la Shepton Mallet, ambalo huandika habari za mji wake huo huko Somerset, walitafsiri vibaya kwamba alikuwa akipiga saluti kushangilia.
Loxton anasema sasa ameelezwa kwamba huduma zake kwa mmoja wa wakurugenzi wa mazishi haihitajiki tena sababu ya shinikizo la vyombo hivyo vya habari.
Alisema: "Kulikuwa na joto sana siku hiyo Juni na nilikuwa nikichimba kaburi la mmoja wa marafiki zangu wa zamani.
"Mpigapicha alinifuata na kuniuliza kama ingekuwa sawa kunipiga picha. Jua lilikuwa likinipiga machoni hivyo nikainua mkono wangu kujikinga nisiathirike macho.
"Baadhi ya watu wali walifikiri nilikuwa napiga saluti na wakaandika kwenye gazeti la mjini humu.
Baada ya hilo nikagundua ningepoteza kazi kutoka kwa mmoja wa wakurugenzi wa mazishi hivyo niliwaita na kuwauliza kilichokuwa kinaendelea.
"Walinieleza kwamba walimpata mtu mwingine kutokana na usikivu wote kwenye vyombo vya habari.
"Nimeumizwa mno, nimechanganyikiwa. Sikupishana nao neno lolote kwa kipindi cha miaka 30 iliyopita. Nilifanya kazi nzuri na hawakuwa na lolote baya la kusema kuhusu kazi yangu."
Picha hiyo, iliyochapishwa katika Jarida la Shepton Mallet Julai, ilipigwa na mpigapicha Jason Bryant kwa ajili ya kipengele cha 'picha ya wiki' kwenye jarida hilo.
Ilitazamwa na zaidi ya watu 15,000 wote kwenye jarida hilo na katika mtandao.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4605

Trending Articles