Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4593

BINTI ALIYEMWAGIWA TINDIKALI ZANZIBAR KUKAA NA BANDEJI MASAA 23 KWA SIKU....

$
0
0
KUSHOTO: Moja ya mitaa ya Mji Mkongwe ambako shambulio hilo lilitokea. KULIA: Kirstie Trup akionesha majeraha yake kifuani.
Mwathirika mmoja wa shambulio la tindikali la Zanzibar bado analazimika kufungwa bandeji ya presha kwenye majeraha yake makubwa kwa masaa 23 kwa siku, imefichuliwa juzi.
Kirstie Trup, ambaye ndiyo kwanza alikuwa ameanza chuo kikuu, ataendelea kukaa na bandeji hizo kwa mwaka mmoja kupunguza maumivu na kudhibiti makovu.
Lakini miezi minne baada ya shambulio hilo, watuhumiwa bado hawajakamatwa ama kushitakiwa.
Kimiminika kutoka kwenye betri la gari, ikiwamo tindikali sulfuriki, ilimwagwa kwa Kirstie na Katie Gee, wote wenye umri wa miaka 18, wakati walipokuwa walipojitolea kama walimu kwenye kituo cha yatima kinachohusiana na Kanisa la Anglikana katika kisiwa hicho.
Wasichana hao kutoka North London walilengwa na wanaume wawili wakati wakitembea kurejea kutoka katika mgahawa mmoja kwenye kisiwa hicho chenye waumini wengi wa dini ya Kiislamu, Agosti 7, mwaka huu.
Juzi baba wa Kirstie, Marc Trup, na Doug Morris, mpenzi wa mama yake Katie, Nicky Gee, walielezea kuchanganyikiwa kwao kufuatia kasi ndogo ya maendeleo ya kesi yao. Waliitaka Serikali kuweka shinikizo zaidi kwa mamlaka husika nchini Tanzania, ambazo zina mamlaka yote katika kisiwa hicho.
Mzee Trup, mwenye miaka 51, daktari wa meno milionea, alisema binti yake alikuwa 'akiendelea vema kimwili na kiakili' baada ya kupata majeraha makubwa ya moto katika bega lake na mgongoni.
Alieleza: "Kirstie anaendelea vema, amehamishiwa chuo kikuu.
"Bado anapatiwa matibabu katika hospitali moja ya jirani. Analazimika kuvalia vazi la mgandamizo juu ya majeraha yake ya moto, ambalo analazimika kulivaa masaa 23 kwa siku kwa kipindi cha mwaka mmoja.
"Huwa anakwenda hospitali mara moja kwa wiki kwa kuchekiwa majeraha yake ya moto, lakini anaendelea vema kimwili na kiakili - anaonekana kuendelea vizuri."
Lakini aliongeza kwamba bado ana 'wakati mgumu'.
Mzee Morris alisema alitarajia Wizara ya Mambo ya Nje 'ingeruka na kuvuka mawimbi makubwa' kuwafikisha watuhumiwa kwenye mkono wa sheria lakini hilo halikuonekana kuwa 'na hisia zozote la uharaka kuhitimisha suala hilo'.
Mzee Trup aliongeza: "Hakika nimesikitishwa na mamlaka za Tanzania. Nadhani wanatarajia kwamba hili litafifia na kutoweka kabisa.
"Wizara ya Mambo ya Nje imekuwa ikitutumia baruapepe, lakini baruapepe hizo zimekuwa zikieleza kitu hicho hicho kila wakati na wanaonekana kudhani kwamba Wizara ya Mambo ya Nje ya Uingereza ina uwezo wa kushawishi, ina sauti, lakini dhahiri hakuna kati ya hayo linalosaidia sababu hatupati maendeleo yoyote kwa namna yoyote.
"Ningependa kuona yeyote aliyemwaga ile tindikali akifikishwa katika mkono wa sheria, siilaumu nchi hiyo, silaumu dini hiyo. Namshutumu mtu aliyefanya hivyo. Anahitajika kufikishwa katika mikono ya sheria.
"Zaidi ya yote, wasichana hao wanataka kujua kwanini aliwafanyia hivyo na tungependa kufahamu kwanini alifanya hivyo. Lilikuwa la kijamii, ilikuwa ni kitu cha kidini? Hatujui kwanini mtu huyo alifanya hivyo."
Polisi wa Zanzibar wamewahoji watu kadhaa, wakiwamo mashuhuda, na inaaminika kuwa wamemtambua anayeshukiwa kufanya shambulio hilo.
Lakini Trup alisema bado kuna mkanganyiko kuhusu jinsi ya kupatikana picha ya mshukiwa huyo ili binti zao waweze kumtambua kama ndiye au la.
"Picha haiwezi kutumwa kwa mfumo sahihi ambao unakubalika na Interpol, au mamlaka za Uingereza, na kama matokeo ya kwamba hakuna yeyote aliyekwisha kuiona picha hiyo," alisema.
Morris alisema Katie ni 'wa ajabu...imara sana kiakili na ndio kwanza anaendana na taratibu za tiba'.
Aliongeza: "Uhalifu huu hauwezi kuachwa bila kuadhibiwa, kwa ajili ya wasichana hao zaidi kama ilivyo kitu kingine chochote.
"Hii ni aina gani ya ujumbe, kwamba unaweza kufanya chochote cha kutisha, unaweza kufanya lolote baya, na ukaweza kukwepa bila kuadhibiwa?"

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4593

Trending Articles