Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4503

MAMIA WAJITOKEZA DAR KUMZIKA MWANAFUNZI ALIYEUAWA NCHINI KENYA...

$
0
0
Jeneza lenye mwili wa Jerry Mruma likishushwa kaburini wakati wa mazishi kwenye makaburi ya Kinondoni, Dar es Salaam jana.
Waziri mstaafu Cleopa Msuya jana aliongoza mamia ya watu waliojitokeza jijini Dar es Salaam katika maziko ya mwanafunzi wa kitanzania aliyeuawa  Nairobi, Kenya, Jerry Mruma (23).

Viongozi wengine waliokuwepo ni pamoja na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,  Goodluck ole Medeye na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Profesa John Nkoma.
Maziko hayo yalifanyika katika makaburi ya Kinondoni na yalitanguliwa na ibada kwenye Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Mbezi Beach,  Dayosisi ya Mashariki na Pwani.
Mchungaji wa Usharika, Allen Mbiso katika ibada, alitaka waumini pamoja na watanzania  kuwa na imani na kushinda ubaya kwa wema. Alisema kufanya hivyo, kunaongeza baraka kutoka kwa Mungu.
Baadhi ya wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Marekani (USIU) tawi la Nairobi alikokuwa akisoma Jerry, walikuwa miongoni mwa walioshiriki maziko.
Balozi wa Vijana wa Jumuiya ya Afrika Mashariki,  Raymond Maro aliyehitimu hivi karibuni chuoni hapo, alisema taifa limepoteza mtu aliyekuwa na malengo makubwa ya kimaendeleo.
Alimtaja kwamba  alikuwa mfano mbele ya wanafunzi wenzake hasa kutokana na uwezo wake mkubwa wa uelewa wa masuala mbalimbali ya msingi.
Alisema hata ilipofika wakati wa majadiliano juu ya masuala mbalimbali yaliyohusisha wataalamu wenye uwezo mkubwa,  aliwaokoa kwa kutoa michango iliyozaa matunda ndani ya mijadala hiyo.
"Ukweli Taifa limepoteza mtu makini na kwa wanafunzi waliobaki chuoni naamini kifo hiki kwao ni pigo kubwa," alisema Maro.
Jerry, ambaye alikuwa akisomea Shahada ya Uzamili ya Utawala wa Biashara (MBA) aliuawa wakati akitoka kwenye hafla ya Usiku wa Mtanzania mjini Nairobi. Mwili  wake ulipatikana mwishoni mwa wiki iliyopita.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4503

Trending Articles