Al Qaeda imetoa toleo la hivi karibuni kabisa la jarida lake la propaganda linalochapishwa kwa lugha ya Kiingereza likielekeza wanaotaka kuwa askari jinsi ya kulipua magari yaliyoegeshwa na kusababisha ajali za barabarani.
Tawi hilo lenye nguvu zaidi la Al Qaeda la harakati za Kiislamu katika Peninsula ya Uarabuni, au AQAP, lilichapisha toleo hilo la kumi linalotoka mara nne kwa mwaka linaloitwa Inspire kwenye tovuti za kijeshi mwezi huu.
Sambamba na vidokezi hivyo kuhusu ugaidi, pia limeionya Ufaransa kuondoa majeshi yake nchini Mali na orodha ya watu 11 maarufu katika nchi za Magharibi, akiwamo mwandishi Salman Rushdie, ambaye linasema 'wanasakwa wakiwa hai ama wafu kujibu mashitaka dhidi ya Uislamu' na kuweka makala za kuwakumbuka 'mashahidi' ambao walikufa kwa sababu yake.
AQAP, lenye makao yake katika taifa maskini, lisilofuata sheria la Yemen, hapo awali lilipanga kutungua ndege za mashirika ya kimataifa.
Linaonekana na serikali za Magharibi kama hatari kwa mataifa Ghuba yanayozalisha mafuta na njia kuu za usafirishaji mafuta ghafi baharini.
Katika kipengele kilichopewa kichwa 'anzisha jihad', jarida hilo limetoa vidokezi vya jinsi ya kuwasha moto magari yaliyoegeshwa, ikiwamo ushauri kama 'usijimwagie petroli mwenyewe', na kupendekeza kumwaga mafuta katika miinuko ya barabarani ili kusababisha magari yagongane.
Tahariri katika jarida hilo iliionya Ufaransa kusitisha uvamizi wake wa kijeshi nchini Mali, ikilinganisha na ule uliofanywa na Marekani katika Afghanistan na Iraki, ambao limesema imewafanya 'wang'ate vidole vyao kwa majuto'.
Jarida hilo pia limewataka wapiganaji kuwashambulia watu 11 maarufu katika nchi za Magharibi, wakiwamo Rushdie, ambaye kitabu chake cha 'The Satanic Verses' mwaka 1988 kilionekana na Waislamu wengi kama kumkashifu Mungu.
Miongoni mwao ni mwanasiasa wa Uholanzi Geert Wilders na mwanaharakati mwenye asili ya Canada na Somalia Ayaan Hirsi Ali, wote wapinzani wakubwa wa Uislamu, na Mchungaji wa Marekani Terry Jones, ambaye aliandaa uchomaji wa nakala za Korani.
Katika makala iliyochomoza, iliyopewa kichwa 'No Parking! Are There Any Safe Parking Lots Out There,' mwandishi aliyejitambulisha kama Ibnul Irhab anaelezea taratibu hatua-kwa-hatua za kuchoma moto magari kadhaa katika eneo moja, maegesho ya wazi, na kufanya mlipuko mkubwa mno.
"Watu wa Magharibi lazima waonje ladha ya moto. Lazima walipe kwa kulipua na kuchoma makazi ya kaka na dada zetu Waislamu' na Kurani yetu Tukufu. Kwa kuteketeza misitu, mashamba na nyumba, tafadhali rejea Toleo Namba 9," mwandishi huyo ameandika.
"Mahitaji yetu makubwa ni mafuta ya kupikia, ukurasa huu wa dokezi unasema, kufanya maangamizi katika barabara kuu zenye kona kali.
"Leo tuna kitu kipya kwa ajili yako, MAGARI. Magari ni rahisi kuchoma. Na sehemu rahisi ni, magari yanahitajika kuegeshwa mahali fulani, sawa? Ni salama kiasi gani sehemu fulani, hasa katika maeneo yaliyotelekezwa?
Maelekezo mahsusi ya Irhab kufanya mipango hiyo ya kutisha ikiwamo, 'kusaka magari yaliyotelekezwa kwenye maegesho,' 'kukwepa kamera za CCTV au maeneo ambapo watu wanaweza kukuona' na 'kumwagia petroli katika gari (magari), usisahau matairi. Unaweza kumwaga kwa mstari kutoka kwenye gari hilo.'
Makala nyingine ya kutisha ilipewe kichwa 'Causing Road Accidents,' iliyoandikwa na mwandishi aliyejitambulisha tu kwa vifupisho AQ Chef, imefafanua jinsi, 'kufuata maelekezo rahisi,' wewe, pia, 'unaweza kufanya uvamizi wa kuua.'
"Hakuna ulipizaji kisasi wa ana kwa ana, tega tu na toweka," inaelezea makala hiyo, ambayo machungu yake yanabainisha jinsi ya kuterezesha barabara zenye umande kwa kutumia mafuta hivyo kufanya magari kuserereka porini na kupinduka.
AQAP limeendelea kuchapisha jarida hilo mara nne kwa mwaka, hata baada ya mmoja wa waandishi wake wakuu, Samir Khan mwenye miaka 26, kutoka North Carolina, kuwa ameuawa katika shambulio la Septemba 2011 nchini Yemen sambamba na mchangiaji mwenzake Anwar al-Awlaki.
Watu kadhaa katika Marekani na Uingereza waliofungwa kwa kuhusika na makosa ya ugaidi wamekutwa wakimiliki nakala za jarida hilo.
Desemba mwaka jana mhitimu kijana ambaye kaka zake wanatumikia vifungo gerezani kwa kupanga shambulio la ugaidi kwenye Soko la Hisa la London, alihukumiwa kifungo jela kwa kufungua mtandao wa Al-Qaeda katika simu yake ya mkononi.
Ruksana Begum, mwenye miaka 22, ambaye ana shahada ya daraja la kwanza ya Uhasibu, ana matoleo mawili ya Inspire, zikiwamo makala kama 'Targeting the populations of countries that are at war with the Muslims'. (Kulenga idadi ya watu ya nchi zilizo katika vita na Waislamu).
Kaka za Begum, Gurukanth Desai, miaka 30, na Abdul Miah, miaka 25, walihukumiwa vifungo vya miaka 12 na 16 Februari, mwaka jana kwa kushiriki kwao kwenye mpango huo.
Oktoba mwaka jana, mwanafunzi alikamatwa kwa jaribio la kulipua Hazina ya New York akilitaja jarida hilo kama kichocheo cha mipango yake hiyo ya hatari.
Quazi Nafis, mwenye miaka 21, alijifunza jinsi ya kutengeneza bomu kutoka katika makala ndani ya jarida la Inspire.
Moja ya matoleo ya jarida hilo yalielezea jinsi ya kutengeneza bomu linalolipuliwa kwa rimoti pamoja na orodha ya vitu vinavyohitajika na vifaa ikifuatiwa na maelekezo kwa njia ya picha.
Toleo jingine lilielekeza njia nzuri ya kuendelea mkakati wa jihad kuwa ni kuwafyeka watembea kwa miguu katika gari aina ya pick-up.
Mafunzo ya kutumia bunduki na vidokezi vya kuja kuwa 'muuaji wa mjini' pia zinapatikana kirahisi kwenye jarida hilo la ugaidi katika mtandao.