Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4510

KILIO CHA WAKULIMA CHAMPONZA WAZIRI WA FEDHA...

$
0
0
Dk William Mgimwa.
Baada ya CCM kusema itamwomba Rais Jakaya Kikwete aruhusu baadhi ya mawaziri wake wafike mbele ya Kamati Kuu ya chama hicho kuhojiwa, wimbi hilo sasa limemkumba Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa.

Wakiwa katika ziara ya kuiimarisha chama, kukagua maendeleo na kusikiliza kero za wananchi katika mikoa ya Kusini, viongozi wa juu wa CCM wameonekana kukerwa na jinsi wananchi wanavyotelekezwa na baadhi ya mawaziri na hivyo kuamua waitwe kujieleza.
Jana CCM iliongeza idadi ya mawaziri hao na kuwa wanne, akiongezeka Dk Mgimwa katika orodha inayojumuisha Waziri wa Kilimo, Christopher Chizza, Naibu wake, Adam Malima na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa kwa kushindwa kuwajibika vizuri katika nafasi zao.
Waziri Mgimwa mwenye dhamana ya fedha atatakiwa kujieleza kuhusu wakulima kutolipwa fedha wanazodai baada ya kuiuzia Serikali mahindi.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, alitoa kauli hiyo kwenye mkutanowa hadhara katika kijiji cha Masangu, kata ya Magagula, wilayani Songea.
Alisema wananchi wanalalamika hawajalipwa fedha zao baada ya kuiuzia Serikali tani 50,000 za mahindi kwa Sh 500 kwa kilo, sawa na zaidi ya Sh bilioni 20, jambo ambalo limefanya washindwe kufanya shughuli za maendeleo.
Alisema hayo si maelekezo yake bali anatekeleza maelekezo yaliyotolewa na Mkutano Mkuu wa Nane wa CCM ambao ulioagiza chama kuisimamia Serikali yake. 
Kinana alisema ataomba kibali kwa Rais Kikwete kumtaka Waziri wa Fedha afike kwenye kikao cha Kamati Kuu mwezi ujao Dodoma ili kutoa maelezo ya kuridhisha kuhusu malipo ya wakulima hao na wasafirishaji wa mahindi.
“Sifanyi hili kwa ajili yangu bali ni katika kutekeleza maagizo ya CCMyaliyotolewa kwenye mkutano wa Novemba mwaka jana,” alisema Kinana.
Alisisitiza kuwa hatanii katika hilo na ni lazima viongozi wawajibike kwaniwalikubali kupokea madaraka na hakuna aliyekataa kushika madaraka hayo.
“Ninaomba waandishi wa habari mnisikilize kwa makini, kwamba ni lazima Waziri wa Fedha aje atoe maelezo kuhusu kuchelewesha malipo ya wakulima wa mahindi waliokopwa na Serikali,” alisema Kinana.
“Natoa taarifa hii mapema ili ajiandae, kwani kuna muda wa kutosha hadi Desemba wakati Kamati Kuu itakapokaa, aandae maelezo ya kwa nini wakulima wa mahindi wanakopwa bila kulipwa,” alisema.
Kinana alisema ni lazima kubanana, kuulizana maswali magumu na kuwajibishana, kwani viongozi wote walikubali kutumikia wananchi na kuondoa kero zao.
Alisema si nia yake, mtu kutokana na maelekezo hayo kama akishindwakuyasema atakuwa hafai kuwa Katibu Mkuu wa Chama.
Licha ya Serikali kubadili muda wa bajeti kutoka Juni na kuwa Aprili ili fedha ziwahi kutolewa na kutumika kwa shughuli za maendeleo ikiwamo ya kulipa wakulima, alishangaa fedha kutotolewa hata Novemba.
Alisisitiza kupatikana maelezo ya kutosha vinginevyo uamuzi mgumu utachukuliwa kwa lengo la kukomboa Watanzania ambao wanakopwa mazao.
Alisema viongozi wakiwamo wakuu wa wilaya, wenyeviti wa halmashauri, wakurugenzi na wananchi wanalalamika kwa nini hadi leo hii fedha hazijatolewa wakati zilitakiwa kutolewa Julai.
Awali Mbunge wa Peramiho, Jenister Mhagama (CCM), alimwomba huku akimpigia magoti kuhakikisha anaibana Serikali ili ilipe fedha za wakulima kwani hivi sasa hawajui la kufanya huku msimu wa kilimo ukikaribia kuanza.
“Nakuomba wewe ili uielekeze Serikali iwaonee huruma wakulima wangu wa mahindi ambao wamekuwa wakitaabika kwa kutolipwa fedha zao za mahindi yaliyochukuliwa na Serikali kwa kipindi kirefu sasa,” alisema Jenister.
Mapema wiki hii akihutubia mkutano wa hadhara wilayani Namtumbo, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, alisema mawaziri watatu  wanatakiwa kuwajibishwa kutokana na kushindwa kutatua kero za wananchi.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4510

Trending Articles