Akiwa na umri wa miaka 53, Jean Claude Van Damme ameonesha kwamba bado wamo kwa kufanya vitu visivyo vya kawaida.
Nyota huyo wa filamu kutoka Ubelgiji ameibuka kivingine pale alipofanya mambo mazito kwenye tangazo la magari mapya ya Volvo ambapo ameonekana akiwa amekaa katikati ya malori mawili yanayotembea kwa kasi barabarani.
Van Damme ambaye alipachikwa jina 'Misuli kutoka Brussels' anatarajiwa kuja kivinginge katika filamu yake mpya ya Enemies Closer inayotarajiwa kuingia mitaani mwezi ujao.
Filamu hiyo ni baada ya ile iliyotikisa ulimwengu mwaka jana akicheza sambamba na Sylvester Stallone, Bruce Willis na Arnold Schwarzenegger iliyofahamika kwa jina la The Expendables Two.