![]() |
Dk Edmund Sengondo Mvungi. |
Habari zilizotufikia hivi punde zinasema kwamba mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Dk Edmund Sengondo Mvungi, amefariki dunia leo mchana katika hospitali ya Milpark iliyoko jijini Johannesburg, Afrika Kusini alikokuwa amelazwa.
Taarifa za Mhadhiri huyo Mwandamizi wa Sheria katika Chuo Kikuu cha Bagamoyo, kufariki dunia zilianza kusambaa mapema leo mchana.
Mmoja wa ndugu wa marehemu ambaye hakutaka kutaja jina lake alithibitisha juu ya kifo hicho kwa njia ya simu.
Kwa kifo hicho washukiwa wa shambulio dhidi yake ambao bila shaka wangefikishwa mahakamani wangeshitakiwa kwa tuhuma za shambulio na kujeruhi, hivi sasa watakuwa wakikabiliwa na tuhuma za mauaji.