Jamaa karudi nyumbani usiku wa manane na kukuta miguu minne ikiwa imechomoza kwenye shuka chumbani mwake. Bila kuuliza, jamaa akachukua rungu na kuanza kuponda-ponda ile miguu kwa wivu. Katika kupunguza hasira zake jamaa akaamua kwenda kukaa sebuleni. Kwa mshangao akamkuta mkewe kajilaza kwenye kochi na kuhoji kulikoni? Mkewe akajibu: "Wazazi wako wamekuja ghafla jioni hii nikaamua kuwapisha kitandani kwetu!" Duh...
↧