Wakati jamii ikiendelea kuamini kuwa mikojo ya binadamu inayohifadhiwa kwenye makazi ya watu kwa ujazo wa mapipa, ndoo na chupa, inatumika kwa ushirikina, wezi wa milango na madirisha katika majengo mbalimbali nao wameendelea 'kuliza' watu kwa kuitumia kutekeleza wizi huo, bila mbinu yao 'kushitukiwa'.
Imebainika kuwa mbinu hiyo ya wizi imekuwa ikitumika kwa miaka mingi, licha ya wanaoibiwa na wanajamii wengine kutoigundua mapema.
Aidha, imekuwa ikiwaacha njia panda wanaoibiwa wasijue ni kwa jinsi gani milango na madirisha ya nyumba zao yameng'olewa kutokana na ukweli kwamba, wizi unafanyika bila kelele wala vishindo.
"Kwa saa kadhaa unashangaa madirisha manne au matano yameng'olewa na kuondolewa katika eneo la nyumba yalipoibwa. Si jirani wala viongozi wa mitaa watakaokwambia kuwa walisikia kelele za kuvunjwa kwa jengo lako, ushahidi huo hawatakuwa nao kwa sababu hakuna kishindo watakachokuwa wamekisikia.
“Na ukienda kuripoti Polisi faili litaandikwa wizi au kuvunja na kuiba kwa mazingira ya kawaida bila kufanya uchunguzi," mmoja wa watu waliowahi kufanyiwa wizi wa aina hiyo Mbezi Louis, Dar es Salaam alieleza.
Mtu huyo alidai alibaini kuibiwa kwa mkojo kwa sababu ya harufu iliyokuwa ikitoka kwenye upande mmoja ulipo ukuta ambako madirisha mawili yaling'olewa.
Alieleza kuwa hisia za kuwa ni mkojo hakuzipata mara moja ila baada ya kutokea wizi wa aina hiyo katika maeneo mengine ambayo nayo yalihusishwa na njama za kishirikika kutokana na kuwa na harufu ya mkojo.
Imebainika kuwa, wizi huo umekuwa ukikua zaidi kadri biashara ya madirisha na milango iliyokwishatumika inavyozidi kukua huku mamlaka mbalimbali za ulinzi na usalama zikiendelea kutoamini kama ni kweli mbinu hiyo inatumika.
Muuzaji mmoja wa milango na madirisha yaliyotumika alimwambia mwandishi kuwa milango na madirisha mengi wanayoletewa yanang’olewa kutoka kwenye majengo mapya na kwamba wanaoyaiba hutumia mkojo kulainisha kuta ili iwe rahisi kuyaachanisha na mchanga wenye saruji uliotumika kuyashikilia.
Kaimu Mkurugenzi wa Huduma ya Uchunguzi wa Sumu na Uchambuzi wa Vielelezo (Forensic and Toxicology services) kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu, Theresia Kahatano, alisema kuwa mkojo unaweza kuharibu jengo, lakini ofisi yake haijafanya utafiti huo wa kina kutokana na ukweli kwamba haijawahi kukutana na suala linalowahitaji kuchunguza kidhibiti kilichoathiri jengo.
"Hata mtu wa kawaida asiye na elimu ya kemia anaweza kukwambia kuwa mkojo unaharibu kuta kutokana na kuziozesha na kuzichimba, lakini, kwa kufuata utaratibu wa kitafiti, siwezi kujibu chochote kwa sasa kwa kuwa hatujafanya utafiti huo kujua kiasi cha athari kinachoweza kusababishwa na mkojo katika jengo," alisema na kuongeza;
"Suala kama hilo lina mambo mengi kwa sababu najua ni kweli mkojo unanyausha hata mazao tena kwa haraka lakini, kwa saruji iliyochanganywa na mchanga ni lazima tutafiti ili kujua ni kwa muda gani unaweza kuharibu na kitu gani kwenye mkojo kinaweza kufanya hivyo, vinginevyo unaweza kukuta kuna kemikali nyingine inaweza kuchanganywa ili kufanya uharibifu huo kwa haraka,” Kahatano alifafanua.
Alisema hata kama wezi wanatumia mbinu hiyo, kugundulika hadi suala hilo litufikie sisi ili tulifanyie kazi itaweza kuchukua muda kutokana na mazoea ya watu kupuuza mambo kwamba hata wakinusa harufu ya mkojo wataendelea tu na shughuli zao hadi jambo kubwa litendeke.
Ofisa Upelelezi wa Kanda Maalumu ya Kipolisi ya Dar es Salaam, Ahmed Msangi alisema hakuna kitu kama hicho ila ni maneno ya watu.
"Huo mkojo utatoka wapi wa kuweza kuozesha jengo la mtu? Na kama hilo lipo basi sijalisikia,"alihoji na kusema.