![]() |
James Mbatia. |
Wakati Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiweka hadharani majina ya wajumbe wa Tume ya Taifa ya Kuchunguza Matokeo ya Kidato cha Nne jana, katika hali ya kushangaza, wadau muhimu wa elimu waliokuwa wameteuliwa wamejitoa.
Wajumbe waliopewa heshima hiyo ya kusaidia kutafuta sababu za matatizo ya elimu na jinsi ya kuyatatua, lakini wakaikataa, ni Mbunge wa Kuteuliwa James Mbatia na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Ezekiel Oluoch.
Wawili hawa ni watu muhimu ambao Taifa lingetarajia kupata mchango wao muhimu ndani ya Tume hiyo, hasa kwa kuzingatia kuwa Oluoch kitaaluma ni mwalimu na Mbatia aliwasilisha hoja katika Mkutano wa 10 wa Bunge hivi karibuni akilalamikia matatizo ya elimu nchini.
Mbatia katika hoja yake kwa waandishi wa habari jana, alisema kwa kuwa hadi jana hakuwa amepata taarifa ya maandishi kuhusu uteuzi wake, asingeweza kutamka kama amekubali au la, hadi atakapokuwa amepata maandishi hayo akisema atakapoyapata ndipo “nitafanya uamuzi kwa maslahi ya pamoja ya Watanzania.”
Hata hivyo, habari za uhakika kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, zilisema Mbatia alifahamishwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Peniel Lyimo kwa njia ya simu afike Ofisi ya Waziri Mkuu achukue barua yake ya uteuzi kama walivyofanya wajumbe wengine.
Oluoch alipotafutwa azungumzie uamuzi wake wa kujitoa kwa mujibu wa barua aliyoiwasilisha Ofisi ya Waziri Mkuu, alisema yuko mkutanoni akaomba apigiwe baada ya nusu saa na ilivyofanyika hivyo, alikata simu kila alipopigiwa.
Uamuzi wa viongozi hao, unatia shaka kama kweli wako tayari kuisaidia nchi katika kutafuta kiini cha matatizo yaliyomo katika sekta ya elimu nchini na kuyatafutia ufumbuzi hasa wanapokuwa wamepewa fursa hiyo ndani ya Tume na kukataa kuitumia.
Tume hiyo inayoanza kazi wiki ijayo ina wajumbe 15 kutoka Tanzania Bara na Tanzania Visiwani, ikiongozwa na Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu (TCU), Profesa Sifuni Mchome na inatarajiwa kufanya kazi kwa wiki sita.
Akizungumza na wajumbe hao ofisini kwake Dar es Salaam jana, Pinda alitaja wajumbe wengine kuwa ni wabunge Bernadetha Mshashu (Viti Maalumu) ambaye ni Makamu Mwenyekiti na Mbunge wa Rufiji, Abdul Marombwa wakiwakilisha Bunge.
Wengine ni Profesa Mwajabu Possi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Makamu wa Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Honoratha Chitanda, Katibu wa Umoja wa Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania (TAHOSSA), Daina Matemu na Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Shule na Vyuo Binafsi nchini (TAMONGSCO), Mahmoud Mringo.
Wengine ni Mwenyekiti wa Twaweza, Rakesh Rajani ambaye alipata kuwa Mkurugenzi wa taasisi ya HakiElimu, Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kikristo ya Huduma za Jamii (CSSC) Peter Maduki, Mratibu wa Mitaala kutoka Taasisi ya Kukuza Mitaala, Kizito Lawa na Mkuu wa Chuo cha Ualimu cha Alharamain, Nurdin Mohammed.
Pinda alitaja wajumbe kutoka visiwani kuwa ni Mwakilishi wa Baraza la Wawakilishi, Suleiman Hemed Khamis, Mwakilishi wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA), Abdallah Hemed Mohammed na Mwakilishi wa Baraza la Elimu Zanzibar, Mabrouk Jabu Makame.
Alisema ameteua wajumbe wengi ili kufanya kazi haraka kwa muda huo mfupi ili Serikali ifanye uamuzi kuhusu wanafunzi waliopata daraja la nne na waliofeli kabisa kwa kupata daraja sifuri, iwapo watarudia mitihani basi wajiandikishe na kujiandaa mapema.
“Jambo hili si la upande mmoja wa shule za kata, Serikali, binafsi au hata zinazoongoza za seminari zote ufaulu wake umekuwa ukishuka kwa miaka mitatu mfululizo, hivyo tatizo hili ni pana sana,” alisema Waziri Mkuu.
Pinda alisema Tume hiyo inatakiwa kubainisha sababu za matokeo hayo mabaya, kushuka kwa kiwango cha ufaulu katika mitihani ya kidato cha nne pamoja na kutathmini nafasi ya Halmashauri katika kusimamia elimu ya sekondari.
“Pia mnatakiwa kutoa mapendekezo ya hatua za kuchukua mara moja kwa wanafunzi 240,903 waliopata daraja la sifuri katika mtihani huo mwaka jana pamoja na zile za kukabiliana na tatizo la mwenendo wa kushuka kwa kiwango cha elimu,” alisisitiza.
Pinda alitoa hadidu za rejea mahususi kuwa ni Mitaala na Muhtasari, kutathmini uwiano wa mitihani inavyotungwa na Baraza la Taifa la Mitihani na uhakiki wa mitihani na maswali unaofanywa na Taasisi ya Kukuza Mitaala.
Pia kutathmini kiwango na mazingira ya ufundishaji kwa kuangalia umahiri wa walimu kumudu maudhui ya masomo wanayofundisha, utoshelevu wa walimu na mengineyo.
Aliwataka pia kuangalia Mfumo wa Upimaji na Tathmini ya Mitihani kwa kuoanisha utungaji wa mitihani na muhtasari iliyotumika kuandaa walimu na mchakato wa usahihishaji.
Kuangalia usimamizi na uendelezaji pamoja na athari ya mfumo wa mikondo miwili uliopo sasa katika shule za Zanzibar na maeneo mengine.
Pinda alitaka wajumbe kufanya kazi kwa kuhoji viongozi na watendaji wa wizara na taasisi mbalimbali, kutembelea shule zilizofanya vizuri na vibaya za serikali binafsi na nyinginezo.
“Pia mnatakiwa kuhoji wanafunzi waliofanya vizuri na vibaya, kupata maoni kwa wadau wakiwamo walimu, wahadhiri, wakufunzi wazazi na wanafunzi na wengineo,” alisema.
Katika hatua nyingine, Mbatia amemwandikia Rais Jakaya Kikwete mapendekezo ya NCCR-Mageuzi kuhusu kuboreshwa kwa elimu ambayo ni kuundwa Tume ya Kudumu ya Elimu, itakayoangalia masuala yanayoweza kusababisha kutetereka kwa ubora huo.
Mengine ni kuimarishwa kwa huduma za ukaguzi wa elimu lakini pia Serikali ikutane na walimu kufanya mazungumzo nao yenye lengo la kujadili ni nini hasa wangependa kuona kinawekwa sawa ili udhaifu uliomo katika mchakato wa ufundishaji na kujifunza kwa wanafunzi shuleni uweze kuondolewa.
Na pia zichukuliwe hatua za dharura kwa matokeo ya kidato cha nne na litolewe agizo la kuwarejesha shuleni ili waanze upya kidato cha tatu au cha nne ikionekana inafaa. “Hii ndiyo njia pekee ya kuwaokoa na matumaini yetu ni kwamba, kwa busara yako utaona hilo linafaa,” alisema Mbatia kwenye mapendekezo yake.