![]() |
KUSHOTO: Joy Grigg. KULIA: Sehemu alipopatikana umbali wa maili tisa kutoka kwake. |
Mama wa watoto wawili ambaye alipotea baada ya kutembea huku akiwa usingizini na kutoka kwenye dirisha lake la jikoni amepatikana - maili tisa kutoka nyumbani kwake.
Joy Grigg, mwenye umri wa miaka 50, alisababisha msako mdogo wa polisi baada ya kutoweka majira ya mapema Jumatano asubuhi.
Mumewe, Richard, mwenye miaka 53, aliamka na kukuta mkewe ameondoka na dirisha la jikoni likiwa wazi.
Alikuwa amepotea kwa takribani masaa 24 hadi mwananchi mmoja alipomwona kwenye ua wa miti iliyooteshwa karibu na Camelford, Cornwall, majira ya Saa 6:30 usiku wa manane siku ya Alhamisi.
Kwa namna ya kushangaza, ilikuwa ni mara ya pili kutoka nje ya shamba la familia huku akiwa usingizini huko Tregeare karibu na Launceston, Cornwall, baada ya kuzurura maili tano kutoka hapo Januari mwaka huu.
Richard, ambaye anaishi Lower Kyrse Farm na Joy na watoto wao wawili wa kiume, Martin mwenye miaka 27, na Geoff miaka 25, alisema: "Ni vema mno kwamba amepatikana.
"Kwa sasa yuko hospitalini, na tunataka tu kurejesha maisha yetu pamoja na kujaribu kuweka vitu katika hali ya kawaida kama vilivyokuwa awali.
"Wote tumefarijika mno na matarajio makubwa sana ya yeye kurejea nyumbani.
"Wote tulikuwa na hofu kuhusu usalama wake na kadri muda ulivyokwenda hofu ilizidi kuongezeka, ingawa yote yamekwisha kwa sasa kwamba amepatikana.
"Ni mtu mwenye hisia kali, mama mwenye upendo na mke na tumefurahi kuungana naye tena."
Joy alipatikana pale wafanyakazi wa uokoaji walipokaribia kusitisha msako wao kupisha giza lililokuwa likitawala.
Msemaji wa timu ya Utafutaji na Uokoaji ya North Dartmoor alisema: "Tulikuwa tena katika eneo la Launceston leo, kusaidia kuendelea kumtafuta Joy Grigg.
"Wakati tukikaribia mwisho wa msako wetu kwa siku hiyo, Joy alionekana salama na mzima."
Richard, mume wa Joy kwa miaka 28, alisema hii sio mara ya kwanza kwa mkewe kupotea.
Alisema: "Alizurura mitaani hapo kabla, takribani wiki sita au saba zilizopita Januari, wakati huo aliishia karibu maili tano kutoka nyumbani.
"Tulifanikiwa kumrejesha nyumbani baada ya mimi kuendelea kumpigia simu yake ya mkononi na hatimaye mtikisiko kwenye mfuko wake ukamuamsha."