![]() |
Warnick (kulia) alihitimu kwenye shule hiyohiyo (pichani) aliyokuja kufundisha. |
Mwalimu mmoja mwenye miaka 22 huko New Jersey amekamatwa Ijumaa kwa tuhuma za kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mmoja wa wanafunzi wake wa kiume mwenye miaka 15 katika Sekondari ya Juu ya Wall Township, ambako ni mwalimu wa Kiingereza wa Darasa la 9.
Mashitaka yaliyofunguliwa dhidi ya Warnick - ambaye licha ya kufundisha Wall Township High School, pia alihitimu kwenye shule hiyo - wanamtuhumu kwa kuchochea mahusiano haramu ya kimapenzi na kuhatarisha afya ya mtoto.
Warnick, ambaye amekuwa akifanya kazi kama mwalimu wa nyumbani majira ya kipindi cha joto tangu Juni, alikamatwa Julai 30 na kuachiwa baada ya kulipa dhamana ya Dola za Marekani 50,000.
Kwa mujibu wa hati ya mashitaka, tukio hilo liliripotiwa Julai 14.
Waendesha mashitaka wa Jimbo la Monmouth hawakuweza kutoa taarifa zaidi.
Charlie Webster, msemaji wa Ofisi ya Mashitaka ya Jimbo la Monmouth, aliwaeleza wanahabari kwamba ofisi yake haitatoa taarifa zozote za jinsi polisi walivyofahamu tuhuma za mahusiano hayo ya kimapenzi kati ya Warnick na mwanafunzi huyo.
"Ni uchunguzi unaoendelea. Mtuhumiwa huyo anatakiwa kujielezea mwenyewe," alisema Webster.
Rais wa Bodi ya Elimu ya Wall Township, Eva Applegate alisema alikuwa akifahamu kuhusu tuhuma hizo shisi ya Warnick, lakini pia alikataa kuzungumzia suala hilo.
"Bodi itajadili suala la mkataba mpya wa mwajiriwa huyo kwa faragha wiki ijayo," aliseme Applegate.
Mwanasheria wa mwalimu huyo, Alton Kenney anasema atakana mashitaka 'sababu, hakika, hana hatia."
Anasema anatarajia Warnick ataachiliwa huru na kurejea kazini kama mwalimu.
Mwanasheria James Maggs, ambaye anaisaidia familia ya mvulana huyo, anasema amepitia 'shambulio hilo la kutisha.'
Warnick anatarajiwa kupanda kizimbani Agosti 6, mwaka huu.