Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4550

AWA MTU WA KWANZA DUNIANI KUTEMBELEA NCHI 201 KWA MIAKA MINNE BILA KUPANDA NDEGE...

$
0
0
Graham Hughes akiinua juu shampeni kushangilia kukamilisha ziara yake Sudani ya Kusini.
Imememchukua Graham Hughes takribani miaka minne kutembelea mataifa 201 na kuwa mtu wa kwanza kuzunguka dunia bila kupanda ndege.

Sasa mashabiki wanaweza kumaliza safari kama hiyo kwa dakika nne bila kuhitaji kuondoka nyumbani.
Mwanaume huyo mwenye miaka 33 anayetokea mjini Liverpool alitumia mabasi, taksi, matreni na miguu yake miwili kusafiri maili 160,000 kwa siku 1,426 - kwa kutumia bajeti ya kamba za viatu ya takribani Dola za Marekani 100 (sawa na Pauni za Uingereza 65) kwa wiki.
Hughes alirekodi safari yake kwa ajili ya simulizi fupi baada ya kuwa ameanza safari hiyo kutoka nyumbani kwake Siku ya Mwaka Mpya 2009.
Hadi Desemba mwaka jana, alivuka mpaka wa kuingia katika taifa jipya la Sudani ya Kusini na kuvungua shampeni kushangilia kumaliza mpango wake huo.
Sasa anahariri video yake hiyo ya siku kadhaa za matembezi kuzunguka dunia, huku akiweka taifa moja katika kila sekunde.
Kwa mikono yake, Hughes alijirekodi mwenyewe akitangaza mahali alipofika kwa ajili ya kumbukumbu za ziara yake, akitekeleza majukumu ya kuhusisha kila kituo kuwa rahisi kidogo - hata kama aliisahau Malta katika jaribio lake la kwanza.
Video hiyo inamuonesha akiwa amesimama kwenye jua huko Amerika ya Kusini na visiwa vya Caribbean, akiota jua huko Canada, na hata kujifanya amekamatwa na wanakijiji katika kisiwa cha Pasifiki ya Kusini cha Vanuatu.
Katika takribani kila picha alivalia kofia yake ya fedora, huku ndevu zake zikiwa zimepunguzwa kwa unadhifu, kwenye misitu na hata sharubu kwa ajili ziara yake nchini Papua New Guinea.
Bila ndege, baadhi ya mataifa ilikuwa vigumu kuyafikia kuliko mengine - lakini si hayo ungeweza kutarajia.
Hughes, ambaye amechangisha takribani Pauni za Uingereza 9,000 kwa ajili ya WaterAid mpaka sasa, alisema ilikuwa rahisi kufika Korea ya Kaskazini, Irak na Afghanistan kuliko ilivyokuwa kufika visiwa vilivyojitenga kama Nauru huko Pasifiki ya Kusini, Maldives na Seychelles.
Ilimchukua majaribio saba kufika Seychelles sababu ya vitisho kutoka kwa maharamia wa Kisomali.
Kwa ujumla alivuka bahari kwa kupata msaada wa meli za mizigo lakini akapata bahati akiwa njiani kuelekea Jamhuri ya Dominika pale meli ya abiria ilipomruhusu kupanda bure.
Hughes alitumia siku nne 'kuvuka bahari ya wazi ndani ya boti iliyokuwa ikivuja' kuweka kufika Cape Verde akitokea Senegal bila njia yoyote ya mawasiliano.
Alifungwa jela kwa wiki moja nchini Kongo kwa kuwa 'shushushu', alikamatwa akijaribu 'kujipenyeza' nchini Urusi na alilazimika 'kuokolewa kutoka kwa Waislamu wenye msimamo mkali na shujaa wa Kifilipino anayeitwa Jenn'.
Sehemu aliyoipenda sana ilikuwa Palau, kisiwa kinachojitegemea katika Pasifiki ya Magharibi.
Picha nyingine kwa kifupi ni pamoja na kucheza na Highlanders wa Papua New Guinea, kujenga urafiki na orangutani huko Borneo, akikatiza nchini Kenya huku akiendesha lori lenye magurudumu 18, kukutana na Waziri Mkuu wa Tuvalu - na 'kutahadharisha watoto wa shule nchini Afghanistan kuhusu hatari za wanaume wenye ndevu'.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4550

Trending Articles