Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4588

MKENYA AHUKUMIWA KIFO KWA KUSAIDIA MAHARAMIA WA SOMALIA KUTEKA, KUUA WATALII...

$
0
0
KUSHOTO: Bi Judoth Tebbutt akiwa amedhoofu baada ya kuachiliwa huru. KULIA: Ali Babitu Kololo akivishwa pingu.
Mfanyakazi wa hoteli moja jana alihukumiwa kifo nchini Kenya baada ya kutiwa hatiani kwa kusaidia kutekwa mtalii wa Uingereza, Bi Judoth Tebbutt wakati wa shambulio ambalo mume wa mtalii huyo alipigwa risasi na kufa.
Ali Babitu Kololo, mwenye miaka 27, alipatikana na hatia ya unyang'anyi wa kutumia nguvu na utekaji nyara kwa lengo la kusababisha mauaji wakati wa shambulio la ghafla la maharamia wa Kisomali mnamo Septemba 2011.
Alihukumiwa adhabu ya kifo lakini anatarajiwa kutumikia maisha yake yote gerezani baada ya Kenya kusimamisha mpango wake wa adhabu ya kifo.
Kololo, Muislamu na baba wa watoto wawili, alitikisika kimya kizimbani huku hakimu Johnstone Munguti akimsomea hukumu hiyo katika hukumu hiyo iliyochukua masaa mawili kwenye mahakama moja iliyoko katika mji wa pwani wa Lamu.
Munguti alisema: "Lazima niseme kwamba nimepewa mamlaka na sheria za Kenya kukuhukumu kifo kwa kosa la kwanza, ambalo ni kwa unyang'anyi wa kutumia nguvu.
"Kwa kosa la pili nakuhukumu kifungo cha miaka saba jela."
Kololo alipelekwa mahakamani hapo akiwa amefungwa pingu baada ya kuwa mtu wa kwanza kutiwa hatiani kwa utekaji nyara wa Tebbutt na kifo cha mumewe.
Wanandoa hao, kutoka Bishop's Stortford huko Hertfordshire, walikuwa wakifurahia mapumziko ndipo kundi la wanaume sita lilipovamia kwenye nyumba yao ndogo ilichojitenga ufukweni saa za mapema Septemba 11, 2011.
Bi Tebbutt, mwenye miaka 58, mfanyakazi wa jamii, alikokotwa kutoka kitandani na kutupwa kwenye boti iendayo kasi ambayo ilimpeleka hadi Somalia.
Alikaa huko zaidi ya miezi sita kama mateka kwenye nchi hiyo yenye vita kabla ya kuachiwa huru mnamo Machi 2012.
Mumewe, mkuu wa uchapishaji, David mwenye miaka 58, alifariki eneo la tukio baada ya kupigwa risasi kifuani wakati akijaribu kumkinga mkewe wakati wa mapigano kwenye ufukwe huo uliojitenga wa Kiwayu Safari Village.
Kololo, ambaye aliwahi kufanya kazi kwenye hoteli moja ya kifahari, alikamatwa siku moja baada ya shambulio hilo na anabaki kuwa mtu pekee kushitakiwa kwa kuhusiana na mkasa huo.
Alikiri mahakamani kwamba alisaidia kuwaongoza washambulizi wa Tebbutt kwenda kwenye nyumba yao ndogo lakini alidai alifanya hivyo kutokana na vitisho baada ya yeye mwenyewe kuwa ametekwa na kundi hilo.
Jana mahakama hiyo ilitupilia madai hayo na kusema ilikuwa wazi alikuwa mfuasi wa sita wa kundi hilo.
Munguti alirejea kwenye ushahidi uliotolewa katika kesi hiyo na Bi Tebbutt, ambaye alieleza jinsi watekaji wake walivyomweleza mfuasi huyo wa sita wa kundi hilo amekamatwa.
Hakimu huyo alisema: "Bi Tebbutt hakuweza kukutambua moja kwa moja, ingawa hakuweza kukuondoa miongoni mwa watuhumiwa.
"Hatahivyo, mmoja wa watekaji wake alisema mtu fulani waliachwa nyuma na kwamba mtu huyo alikuwa tatizo kubwa nchini Kenya.
"Katika ushahidi huo, mtu huyo anaweza kuwa ni wewe tu, sababu hakuna mtu mwingine aliyekuwa amekamatwa na kushitakiwa."
Kololo, Muislamu msalihina, alivalia fulana ya pinki jana huku akiendelea kukataa hatia yake.
Akiielezea mahakama upunguzaji wake mwenyewe makosa, alisema: "Nimemwachia kila kitu Mungu. Nasubiri uamuzi wako."
Aliongeza: "Sikushiriki kwenye shambulio hilo. Upande wa mashitaka umenibambikizia kesi."
Wapelelezi wawili kutoka Makao Makuu ya Polisi Uingereza walikuwa mahakamani hapo jana kufuatilia kesi hiyo.
Wawili hao walikuwa sehemu ya timu iliyokwenda kuwasaidia polisi wa Kenya siku kadhaa baada ya shambulio hilo.
Bi Tebbutt alieleza kwenye kitabu chake jinsi alivyoishi wiki tatu za kwanza za kutekwa kwake akiamini siku moja ataweza kuungana tena na mume wake.
Baadaye aligundua kifo cha mumewe baada ya watekaji wake kuwasiliana kwa simu na mtoto wake wa kiume, Oliver.
Bi Tebbutt baadaye aliachiliwa mnamo Machi 2012 baada ya familia yake kuchangishana fedha za malipo ili kuwezesha kuachiwa mateka.
Mjane huyo alishaelezea hamu yake ya kushuhudia hukumu ya haki ikitendeka.
Hukumu ya kifo ni chanzo cha mabishano nchini Kenya, ambapo wanaharakati wa haki za binadamu wameshauri izuiwe.
Nchi hiyo haijatekeleza hukumu yoyote ya kifo tangu mwaka 1987 na kwa sasa inapitia upya hukumu zake.
Maofisa waliashiria kwamba kuna uwezekano mkubwa kwa Kololo kukwepa hukumu hiyo ya kifo.
Badala yake, inatarajiwa hukumu yake inaweza kubadilishwa na kuwa kifungo cha maisha gerezani.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4588

Trending Articles