Quantcast
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4580

HATIMA YA KESI YA RUSHWA DHIDI YA HAKIMU MKAZI ILALA KUJULIKANA LEO...

Image may be NSFW.
Clik here to view.
Pamela Kalala.
Hatima ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam, Pamela Kalala  anayekabiliwa na kesi ya kuomba rushwa ya Sh milioni tatu, itajulikana leo Mahakama itakapotoa uamuzi kama ana kesi ya kujibu au la.

Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Aloyce Katemana  atatoa uamuzi huo baada ya Taasisi ya Kupambana na Kuzuia  Rushwa (Takukuru), kufunga ushahidi wao.
Endapo Hakimu huyo atapatikana na kesi ya kujibu atapanda kizimbani kujitetea na kama hana kesi ya kujibu ataachiwa huru.
Mshitakiwa huyo anadaiwa kuomba na kupokea rushwa kutoka kwa mke wa mmoja wa washitakiwa ambao alikuwa akisikiliza kesi yao, Josephine Wage ili atoe dhamana kwa mumewe.
Akitoa ushahidi mwishoni mwa wiki, Msajili wa Wilaya wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, Amir Msumi, alidai kuwa alishangaa kuona Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya Ilala, Pamela Kalala, kumfutia dhamana mshtakiwa bila kueleza sababu.
Alidai alipokea barua ya kushughulikia malalamiko dhidi ya mshitakiwa ambayo yaliambatana na barua iliyoandikwa na Josephine, akimlalamikia Hakimu Kalala kufuta dhamana ya mumewe, na mazingira yasiyoridhisha ya uendeshaji wa kesi namba 703 ya mwaka 2008 inayomkabili mumewe.
Hakimu Kalala anadaiwa kuomba rushwa ya Sh milioni tatu kutoka kwa Wage na kupokea Sh 900,000 Februari mwaka jana jijini Dar es Salaam.
Ilidaiwa kuwa rushwa hiyo ilikuwa ni kumshawishi Kalala kutoa uamuzi wa kumpendelea mumewe.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4580

Trending Articles