![]() |
Charles Lutzow (kulia) akiwa na binti yake, Keri Abercrombie. |
Baba mmoja wa Alabama ameungana na binti yake aliyepotea muda mrefu baada ya kuwa ameamini alikufa kwa takribani nusu karne.
Charles Lutzow, kutoka Rockford, na mkewe anayekaribia kujifungua, Stella, walitengana kwa miezi miwili mnamo mwaka 1967. Pale waliporudiana, Stella akajifungua mtoto na kumweleza mumewe mtoto huyo alikufa wakati akijifungua.
Kinyume chake, kumbe alikuwa amempeleka binti huko mwenye afya njema kuasiliwa bila kumweleza mumewe huyo.
Stella alitunza siri yake hadi alipokufa karibu miaka kumi iliyopita, lakini mnamo Desemba binti wa wanandoa hao, Keri Abercrombie akamtafuta na kumpata baba yake mzazi.
Binti huyo ambaye sasa ana miaka 45 alikutana na familia yake hiyo kwa mara ya kwanza wiki hii, na tukio hilo la kusisimua kunaswa na kituo cha WIFR.
"Siwezi kuongea chochote, nimefurahi mno," Keri alikieleza kituo hicho, huku baba yake mwenye furaha iliyovuka mipaka akimkumbatia.
"Niliamini alikuwa amefariki kwa wakati wote huu," Lutzow aliongeza.
Mwanamke huyo alipata taarifa za baba yake kupitia
Masijala ya Kuasili na mtandao wa kijamii wa Facebook.
Baada ya kufikiria kwa zaidi ya miezi, hatimaye akapata nafasi na kumpata kaka yake wa tumbo moja kupitia kwenye mtandao kujieleza yeye ni nani.
"Nilimweleza 'nafikiri mimi ni dada yako' na akashituka 'nini, dada?"
Kisha akampigia simu.
"Nilimwita (baba yangu) na kusema 'hey, nimekupata, wewe ni baba yangu," Keri alisema Jumanne, huku akikutana na wanafamilia wengine.
"Sikujua alikuwa nani," aliongeza Lutzow.
Keri alikulia huko Utah kwa wazazi wake wapenzi waliomuasili na sasa anaishi Alabama. Alihamia Rockford na familia yake mwaka 1985 kujiunga na mwaka wa kwanza wa sekondari ya juu.
Alisema wakati wote alikuwa akifahamu kwamba ameasiliwa.
Keri aliandika kuhusu tukio hilo la kusisismua kwenye Facebook.
"Kuja kugundua kwamba nina familia nzima pale," Keri aliandika Jumanne.
"Nilibarikiwa kupata wazazi wa kuasili wa aina yake. Napenda kumshukuru Mungu, kwa kunipatia familia yangu halisi."
Lutzow alisisimka mno kufuatia uvumbuzi huo, ambao umetokea mwishoni kabisa mwa maisha yake.
"Tulitengana kwa miaka 45, sasa hatimaye tumeungana pamoja, ni Mungu aliyetuleta pamoja," Lutzow aliieleza WIFR.