Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4510

AMUUA MAMA YAKE KWA KUMKATA VIUNGO NA KUVITUPA MITAANI...

$
0
0
KUSHOTO: Tanya Byrd. JUU: Moja ya sehemu za mwili wa mama huyo. CHINI: Bahsid McLean.
Picha ya kutisha imeibuka Jumamosi ikionesha mkazi wa Bronx anayetuhumiwa kuua na kukata viungo mwili wa mama yake, akitabasamu na kuonesha kichwa cha mwanamke huyo aliyekufa.
Bahsid McLean, mwenye miaka 23, amesimama mbele ya kioo cha bafuni akiwa ameshikilia kichwa kilichotapakaa damu cha mama yake, Tanya Byrd, kama tuzo na kutumia simu yake kupiga picha, katika picha iliyovujishwa kwenye gazeti la New York Post.
Bahsid ameshitakiwa kwa mauaji ya Tanya, mwenye miaka 45, baada ya malumbano ambayo mama huyo alimweleza mtoto wake huyo wa kiume kuhama kwenye nyumba yake iliyoko Morrisania, karibu na South Bronx na kwenda kujitegemea.
Ofisa wa Sheria alisema picha hiyo ya kushitusha ni moja kati ya picha kadhaa zilizokutwa kwenye simu ya mkononi ya Bahsid.
"Nimeshindwa kulala sababu ya picha hiyo. Inaonesha kukosa ubinadamu. Inatisha alichomfanyia," chanzo hicho kimelieleza Post.
Polisi imesema kwamba baada ya Bahsid kumchoma visu mwanamke huyo hadi kufa, inawezekana usiku wa Jumamosi au Jumatatu, alikatakata mwili wake kwa kutumia panga na kutawanya viungo vya mwili huo kwenye maeneo mbalimbali ya jirani na Bronx.
Kisha yeye na mwenzake wanadaiwa kufunga sehemu za mwili wa mwanamke huyo kwenye mifuko mikubwa ya taka, baadhi yake ikiwa imefungwa ndani kama mizigo na kuitupa katika maeneo takribani manne tofauti katika Morrisania, ambako waliigundua mapema Jumanne asubuhi kwa kutumia askari wa vikosi vya mbwa.
Bahsid alifikishwa mahakamani Ijumaa kwa unyama wake huo, akidai kwamba 'hakufanya jambo lolote baya.'
Akiwa amevalia mfuko wa taka mweusi wa plastiki wakati wa kusikilizwa kesi yake sababu alikuwa akiendelea kujikojolea, anaendelea kuwa chini ya uangalizi asije kujiua baada ya shambulio hilo la kutisha mapema wiki hii dhidi ya mama yake.
Mtu huyo mwenye matatizo ya akili alimweleza jaji kwamba Tanya alikuwa akikaribia kufa na kwamba alikuwa akijaribu kumsaidia, ingawa haikufahamika alikuwa akitakiwa kufa kwa sababu gani.
Wakili wa Bahsid, Jerry Iannece alisema mteja wake, ambaye anafanyiwa uchunguzi wa akili, alikuwa kwenye matibabu lakini hakufafanua mtu huyo mwenye miaka 23 alikuwa akitibiwa nini.
Gazeti la Daily News liliripoti shuhuda akisema waliona mifuko waliyoitilia mashaka na vitu vya kutisha kwenye mifuko ndani ya gari na kisha kutokomea eneo la tukio katika gari aina ya SUV.
Mwanamke mmoja alisema mguu wa mwanamke ulikuwa ukionekana wazi, ukichomoza kutoka kwenye moja ya mifuko hiyo.
"Ulikuwa ukichungulia kwenye mfuko na dhahiri ulikuwa mguu wa Mmarekani Mweusi," aliieleza WCBS 880.
Mguu wa kulia wa Tanya ulikutwa kwenye Barabara ya Eagle karibu na Mtaa wa 156, wakati kiwiliwili chake kilipatikana Barabara ya Eagle karibu na Mtaa wa 158, mashuhuda walilieleza The Post.
Kicha cha mama huyo kilikutwa katika Barabara ya Cauldwell na Mtaa wa 158. Wachunguzi pia walipata mkono wa mwanamke huyo, ingawa haikufahamika ni wapi.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4510

Trending Articles