![]() |
Papa wakikiwa kwenye mawindo baharini. |
Msichana mmoja 'amekufa papo hapo' baada ya kuchanwa nusu kwa nusu na papa wakati akicheza mchezo wa kuelea juu ya maji karibu na ufukwe katika kisiwa cha maraha kwenye Bahari ya Hindi.
Binti huyo mwenye umri wa miaka 15, alikuwa umbali wa mita 5 kutoka pwani ya kisiwa cha Reunion, kilichopo kando ya ufukwe wa Madagascar, ndipo shambulio hilo la kukatisha uhai lilipotokea.
Dada yake aliyejawa na hofu alikuwa miongoni mwa wote walioshuhudia mwanafunzi huyo wa kike akitoweka chini ya maji majira ya Saa 9 mchana jana.
Mwili wa msichana huyo ulikatwa vipande viwili kwenye pingiti, na kisha sehemu ya mwili huo ukachukuliwa na pap huyo," alisema Gina Hoarau, mkuu wa usalama wa umma katika kisiwa hicho.
Aliongeza: "Wasichana hao walikuwa katika eneo hilo la ghuba ya St Paul ambako kuogelea kumepigwa marufuku. Aliuawa na papa wakati akicheza mchezo wa kuelea kwenye maji si mbali na ufukwe katika kisiwa cha Reunion, ambacho kipo katika Bahari ya Hindi.
Mkuu huyo mwenye umri wa miaka 36 alikuwa kwenye bahari kando ya ufukwe maarufu wa Brisants de Saint-Gilles ndipo papa alipomfukuza mara mbili, na kumshawishi mwogeleaji wa karibu kutoa taarifa pale alipoona damu katika maji.
Waokoaji walijitosa kwenye maji kumsaka muathirika, ambaye alipoteza damu nyingi na ambaye alipatwa majeraha kwenye moyo na kupumua kwa shida.
Walimrejesha ufukweni lakini hawakufanikiwa kuokoa maisha yake.
Papa huyo alikuwa amemng'ata mwogeleaji huyo kwenye mkono na pajani. Mkewe alikuwa ufukweni wakati tukio hilo lilitendeka, na alipatiwa matibabu kutokana na mshituko aliopata.
Shambulio hili hatari la hivi karibuni linakuwa la pili kwenye kisiwa hicho mwaka huu, wakati watu watatu wakiwa wameuawa na papa katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.
Papa si wala-binadamu, lakini wakati mwingine huwafananisha na vyakula vyao, kama sili au kobe, na wakati mwingine huwajeruhi wacheza michezo ya kuserereka kwenye maji," amesema mtaalamu.
Mwaka jana, matukio 78 ya kushambuliwa na papa yaliripotiwa duniani, ambapo manane kati ya hayo yalikuwa ya kutisha.