![]() |
Baadhi ya taksi za nchini Thailand. |
Dereva taksi mmoja wa Thailand amekamatwa kwa mauaji ya raia wa Marekani, ambaye anadaiwa kumuua kwa kushindwa kulipa nauli ya Dola za Marekani 1.50.
Troy Lee Pilkington, mwenye umri wa miaka 51, alichoma kwa kisu hadi kufa pale aliposhindwa kulipia safari aliyofanya kwa kutumia taksi hiyo katikati ya mji wa Bangkok, Thailand Jumamosi iliyopita.
Dereva taksi huyo mwenye umri wa miaka 32 alikiri kuchomoa kisu lake chenye urefu wa inchi 12 kutoka kwenye ala yake na kumchoma mara kadhaa Pilkington pale alipokataa kulipa Baht 51 (sawa na Dola za Marekani 1.60) za nauli.
Mtaalamu wa Marekani Troy Lee Pilkington aliuawa mjini Bangkok baada ya kutokuelewana na dereva taksi mmoja wa mjini humo, alisema Luteni Kanali wa Polisi Teerayut Maiplaeng.
Picha za video kutoka kwenye kamera zilinasa sehemu ya tukio hilo la kikatili, ambalo lilitokea Jumamosi kwenye barabara yenye pilika nyingi mjini Bangkok ya Sukhumvit.
Picha hizo zinaonesha dereva taksi huyo akipepeza kisu chake angani huku mwanaume aliyetambuliwa kama Pilkington, akinyoosha mikono yake na kujaribu kumkamata dereva huyo.
Wanaume hao wawili kisha walitoka kwenye upeo wa kamera, na sekunde chache baadaye dereva huyo aliyetapakaa damu akatokea tena kwenye fremu wakati akitoweka eneo la tukio.
Pilkington, alikuwa akifanya kazi kwenye kampuni ya Marekani ya mashine Caterpillar Inc. na aliishi nchini Thailand kwa takribani miaka mitatu.
Dereva taksi huyo, Chidchai Utmacha, aliwaeleza wachunguzi kwamba Pilkington alimtuhumu kwa kuchakachua mita ya taksi hiyo na kisha kushuka kwenye taksi hiyo wakati ikiwa imesimama kwenye foleni.
Alidai Mmarekani huyo akamrushia kikombe cha kahawa pale alipomdai kiasi hicho cha fedha, ndipo alipotoa kisu chake kutoka kwenye ala na kuanza kumkimbiza Pilkington.
Polisi walimtambua dereva huyo kutokea kwenye picha za video na kumkamata nyumbani kwake siku ya Jumapili.
Chidchai anakabiliwa na mashitaka ya mauaji na kubeba silaha hadharani bila sababu za msingi.