Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4630

MHUDUMU WA KIKE WA NDEGE ADAIWA KUSAFIRISHA PANYA KWENYE NGUO ZAKE ZA NDANI...

$
0
0
Panya wa kufugwa.
Mhudumu mmoja wa ndege ya American Airlines amelishitaki shirika hilo baada ya madai yaliyoibuliwa na mwenzake kwamba alishafirisha panya wake wa kufugwa ndani ya chupi yake na nguo iliyobana kwenye ndege iliyokuwa ikifanya safari za kimataifa.

Mhudumu wa ndege inayoenda Long Island, Louann Giambattista, mwenye umri wa miaka 55, anasema madai hayo yamemsababishia kuwekwa kwenye kitabu cheusi na forodha kwa zaidi ya mwaka mmoja.
Mkongwe huyo aliye kwenye fani hiyo kwa miaka 33 anadai fidia kwa kuumizwa na madai hayo pamoja na kuathiriwa kisaikolojia kutoka kwa shirika hilo.
Februari 2012, rumani mmoja aliripoti kwamba Louann alikuwa na 'uvimbe kwenye mfuko wake' na aliona 'kile alichodhani ni kiumbe hai,' kwa mujibu wa nyaraka zilizofunguliwa kwenye mahakama ya Brooklyn.
Mwenzake mwingine aliripoti kwamba katika ndege iliyokuwa ikielekea Miami siku hiyo, alimwona Louann akimlisha panya wa kufugwa. Louann anadai kwamba mkate uliokuwa ndani ya kikombe cha karatasi haukuwa kwa ajili ya kulishia panya lakini ni kwa ajili yake, na kwamba kikombe hicho alikitumia kuepuka kuonekana asiyezingatia weledi mbele ya abiria.
Kwa mujibu wa nyaraka hizo za mahakama, wenzake kwenye ndege inayoelekea Miami walihisi harufu ya panya na kumkabidhi Louann kwa maofisa wa forodha mara tu ndege ilipotua mjini Florida.
Anasema alihojiwa na begi lake kupekuliwa kwa zaidi ya saa moja, lakini maofisa hao hawakukuta panya wowote.
Kama haitoshi, Louann anadai ndege hiyo iliweka bendera kwenye pasipoti yake kufuatia tuhuma hizo, ikimaanisha kwamba kila safari kupitia forodha inatakuwa mateso ya muda mrefu na wakala wa ICE walimfanyia ukatili na kumtisha kumpekua akiwa uchi, na hiyo ilikaribia kumfanya ashindwe kuripoti kazini."
Kwa mujibu wa ripoti, Louann alikiri kuwa anayependa wanyama, lakini mwanasheria wake anasema mama huyo anafahamu kuna wakati na sehemu maalumu kwa ajili ya wanyama.
"Kila mmoja ana wanyama - Louann anao wanyama wake nyumbani, sio kazini," alisem Stephen Morelli. "Sio mtukutu. Wanamfanya aonekane ni mtukutu."
"Ana wanyama wengi tofauti. Alikuwa na panya - amekufa."
Louann alieleza kwamba madai hayo alikuwa akisafirisha panya kwenye ndege ni 'upuuzi' na 'uongo dhahiri'.
"Hakuna sababu ya kufanya hivyo," alisema. "Watu wanasema, 'Lazima kuwe na sababu' lakini hakukuwa na kitu."
Anasema alikuwa akionesha mfano mbele ya wenzake na kuhojiwa kwenye chumba cha mapumziko ambako wenzake wengine waliweza kushuhudia mahojiano yake.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4630

Trending Articles