Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4529

MAMLAKA YA HEWA YAHADHARISHA MAWIMBI MAKUBWA BAHARINI...

$
0
0
Mamlaka ya Hali ya Hewa  Tanzania  (TMA) imehadharisha upepo kuwapo na upepo mkali baharini unaopiga kilometa 40 kwa saa na mawimbi yenye ukubwa unaozidi mita 2.0.

Taarifa ya hali ya hewa iliyotolewa jana ilisema kwamba maeneo yatakayoathirika na hali hiyo kwa siku tatu kuanzia leo ni Tanga, Dar es Salaam, Pwani, Lindi, Mtwara, Mafia na visiwa vya Unguja na Pemba.
TMA imewataka wakazi wa maeneo husika, na watumiaji wa bahari kuchukua hadhari kubwa na mabadiliko hayo yaliyopo baharini. 
Hali hiyo inatajwa kwamba  inatokana na kuimarika kwa mfumo wa mgandamizo mkubwa wa hewa katika eneo la Kusini-Mashariki mwa Afrika.
Watumiaji wa bahari wanashauriwa kuchukua hatua za kiuasalama kutokana na hali mbaya ya bahari inayotarajiwa  kuwepo.
Hata hivyo, Mamlaka ya Hali ya Hewa imesema inaendelea kufuatilia hali hiyo na itatoa mrejeo. 
Kaimu Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Bandari nchini,  Janeth Ruzangi alisema wamepata taarifa juu ya hali hiyo na kwamba Kitengo cha Usalama Bandarini, kimewaarifu wenye meli kuzifunga vyema kwenye gati.
Kwa upande wake, Ofisa wa zamu wa Kituo cha Utafutaji na Uokozi (MRCC) kilichoko chini ya Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra), Emanuel Lusuva alisema walipata hadhari hiyo tangu wiki iliyopita na wamejiandaa.
Alisema wameshawasiliana na wawakilishi katika pwani ya Tanga na Mtwara wasambaze hadhari hiyo na wazuie vyombo vya usafiri kuingia baharini.
 “Hali ikiwa nzuri baharini huwapa taarifa wawakilishi wetu…kadhalika na hali ikiwa mbaya pia huwasilisha taarifa na kwa vile taarifa hii ya tahadhari tulipewa kuanzia  Ijumaa tayari tulishawasiliana na tumezuia vyombo vya usafiri kwenda baharini,” alisema Lusuva.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4529

Trending Articles