Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4529

MLIPUKO WAMKATA VIGANJA MWENDESHA PIKIPIKI DAR...

$
0
0
Mkazi wa Mbagala Chemichem, Abdul Said ambaye ni mwendesha pikipiki amekatika viganja vya mikono miwili baada ya kulipukiw a na kitu alichopewa kushika.
Hata hivyo Said anashikiliwa na polisi na mwenzake mwingine ambaye hakutajwa jina baada ya kukamatwa katika maeneo ya Mbagala jana saa 6:00 usiku.
Kamishna wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Suleiman Kova, alisema watu hao wawili walikamatwa katika maeneo hayo huku wenzao wawili wakipata upenyo na kukimbia.
Alisema dereva huyo wa pikipiki ambaye alikabidhiwa kitu mkononi ambacho ghafla kililipuka na kumkata viganja vya mikono yote miwili.
Alisema jitihada za kuwatafuta watuhumiwa wengine wawili bado zinaendelea na waliokamatwa wanashikiliwa kwa mahojiano.
Katika hatua nyingine, Kamanda Kova alisema walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa wa makosa mbalimbali ya unyang’anyi kwa kutumia silaha Moshi Omari akiwa na pikipiki aina ya Honda Bajaj yenye namba T607 AQD ambayo ni ya wizi.
“Vilevile katika kuendeleza doria za kuimarisha ulinzi tumewakamata watuhumiwa wawili kwa kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha ambao wameshiriki katika matukio mengi ya uhalifu hapa jijini,” alisema Kamanda Kova.
Aliwataja watu hao kuwa ni Jovin Deofin na Juma Athuman ambao wote ni wakazi wa Kongowe, Wilaya ya Temeke.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4529

Trending Articles