![]() |
Mzee Nelson Mandela. |
Rais mstaafu wa Afrika Kusini, Mzee Nelson Mandela amekimbizwa hospitalini akiwa kwenye 'hali mbaya' saa chache zilizopita kufuatia kurudia kwa maambukizo kwenye mapafu ambayo yalimkumba katika miezi ya hivi karibuni.
Kiongozi huyo wa harakati za kupinga ubaguzi mwenye umri wa miaka 94, ambaye afya yake imekuwa ikizorota katika miaka ya karibuni, ameshalazwa hospitalini mara tatu tangu Desemba.
Mandela alisemekana kupata nafuu lakini hali hiyo ilikuwa 'mbaya sana wakati huu,' msemaji wa serikali alieleza muda mfupi uliopita..
"Hali hiyo ni mbaya wakati huu lakini madaktari wametuhakikishia anaendelea vizuri," alisema msemaji wa rais Mac Maharaj.
Maharaj alisema ndugu wa familia ya Mzee Mandela wameongozana naye kwenda hospitali na wameendelea kuwa kando ya kitanda chake.
Mkewe, Graca Machel, amefuta ratiba yake ya kuhudhuria mkutano wa kujadili njaa mjini London leo na anadhaniwa kuwa amepanda ndege kurejea Afrika Kusini kumuugua mumewe.
Maneno ya taarifa ya serikali, katika matumizi ya neno 'mbaya', ni sababu dhahiri ya kujali kwa watu milioni 53 wa Afrika Kusini, kwake Mzee Mandela anayeendelea kuwa alama muhimu ya mapambano dhidi ya utawala wa miaka mingi wa watu wachache weupe.
Mzee Mandela amekuwa akisumbuliwa mno na matatizo ya upumuaji tangu alipopata maradhi ya kifua kikuu wati wa miaka yake 27 aliyotumikia kifungo chini ya ubaguzi wa rangi.
Madaktari wanatibu jambo hilo kwa tahadhari kubwa, alisema Maharaj, na Mzee Mandela amelazwa hospitalini hapo 'hasa hasa' kumpatia nafasi muhimu ya kupona kabisa.
"Amekuwa akiendelea vizuri. Ni mpambanaji na atakuwa nasi huku akiendelea kupambana," aliongeza Maharaj.
Aliieleza Sky News kiongozi huyo wa zamani alikuwa na fahamu zake, 'anaweza kupumua mwenyewe', na 'anawasiliana' na jamaa zake waliomzunguka kitandani kwake.
Taarifa ya mapema kutoka ofisi ya Rais Jacob Zuma ilisema: "Katika siku chache zilizopita, Rais wa zamani Nelson Mandela amerudiwa na maambukizi kwenye mapafu.
"Asubuhi hii majira ya Saa 7:30 alfajiri, hali yake ilizorota na alihamishiwa katika hospitali moja mjini Pretoria."
Taarifa hii ilisema Mzee Mandela ameendelea kuwa katika hali 'mbaya lakini imara'.
Ilisema Mzee Mandela, ambaye atasherehekea siku yake ya kuzaliwa kutimiza miaka 95 mwezi ujao, alikuwa akipatiwa matibabu ya hali ya juu na 'madaktari wanafanya kila liwezekanalo kumfanya awe na hali nzuri na faraja'.
Zuma alimtakia Mzee Mandela kupona haraka kwa niaba ya serikali hiyo na taifa hilo na kutoa wito kiongozi huyo wa zamani aachwe apumzike.