Quantcast
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4529

TANGAZO LA SHUKRANI...


 SHUKRANI
CASSIUS MGAVINYI BERNARD KIBASSA
05 JULAI 1963 – 12 APRILI 2013

Ilikuwa usiku wa tarehe 12 Aprili 2013 tulipopigiwa simu na kupewa taarifa kuwa mpendwa wetu Cassius hayuko nasi tena. 
Cassius tunajua kuwa kila kizaliwacho hakina budi kufa, lakini tunakiri kuwa tulipata mstuko mkubwa ambao mpaka sasa bado tunaona kama ndoto.  Hata hivyo tukiwa na imani inatubidi kukubali kuwa kila mwana adamu amepangiwa kifo chake, Mapenzi ya Bwana Yatimizwe.
Kwa namna ya pekee tunapenda kutoa shukrani kwa Uongozi na Ofisi ya Bunge Dodoma na Dar es Salaam kwa misaada yote na kwa kushirikiana nasi katikam kipindi hiki kigumu katika matayarisho na hatimaye kumpumzisha katika nyumba ya milele mpendwa wetu Cassius.
Kwa kuwa si rahisi kumshukuru kila mtu, basi familia ingependa kutoa shukrani za pekee kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Mhe. Anna Makinda, Naibu Spika, Mhe. Job Ndugai, Katibu wa Bunge, Mhe. Dkt Thomas Kashililah, Mhe. William Lukuvi (Mb), Mhe. Steven Wassira (Mb), Mhe. Margareth Sitta (Mb), Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Mama Kipa, Mhe. Profesa Msola (Mb) na Mkuu wa Mkoa Iringa, Mama Christine Ishengoma. Vile vile tunapenda kuwashukuru sana ndugu, jamaa, marafiki  na majirani wote wa Dodoma na Dar es Salaam ambao walikuwa bega kwa bega nasi, Baba na Mama Mtenga wa Kikuyu, Jumuiya ya Mtakatifu Matilda ya Dodoma,  Baba Paroko wa Kanisa la Mtakatifu Paulo wa Msalaba Dodoma, bila kuwasahau ndugu, jamaa na marafiki wote wa Iringa mjini na kijijini Nyabula kwa namna ambavyo tumekuwa pamoja mpaka kufanikisha mazishi ya mpendwa wetu Cassius.
Mkesha wa kumaliza msiba utafanyika kijijini Nyabula, Iringa mnamo tarehe 13 Juni 2013 na tarehe 14 Juni 2013 kutakuwa na Misa ya kumuombea mpendwa wetu itakayofuatiwa na kusimika msalaba itakayofanyikia kijijini Malendi, Iringa.  Baada ya hapo tunaomba wote tujumuike kwa chakula cha mchana hapo Malendi, Nyabula.

RAHA YA MILELE UMPE E BWANA, NA MWANGA WA MILELE UMWANGAZIE, APUMZIKE KWA AMANI, AMINA.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 4529

Trending Articles