![]() |
Kainat Soomro. |
Mapambano ya kijasiri ya muathirika wa tukio la ubakaji na genge la wahuni aliyetengwa na kijiji chake nchini Pakistani kwa kuwashutumu wanaodaiwa kumshambulia sasa ni mada ya filamu fupi kuhuzunisha.
Kainat Soomro alipachikwa jina 'kari', au 'bikira mweusi', na familia yake mwenyewe imeamriwa kumuua ili kuwaondolea aibu baada ya binti huyo kusema kuwa alibakwa na wanaume wanne akiwa na umri wa miaka 13 mwaka 2007.
Lakini ndugu wa msichana huyo wamegoma kumwachia kisogo Kainat, na wametakiwa kumsaidia wakati akipiga hatua ya kushangaza ya kupigania haki yake katika sheria fedhuli zinazokatisha tamaa ambazo zimekuwa zikitumika nchini Pakistan kwa karne kadhaa.
Miaka hiyo iliyopita tangu shambulio hilo lisilosahaulika la Kainat imethibitisha kuwepo ugumu, huku familia yake ikimtimuliwa kutoka kwenye kijiji chao, Dadu, katikati ya vitisho vya ghasia na mauaji.
Baba yake na mmoja wa kaka zake walipigwa, wakati kaka yake mkubwa alitoweka kwa miezi mitatu kabla ya kupatikana akiwa ameuawa.
Harakati za Kainat katika kesi hiyo kupitia mfumo wa kisheria ambao umebebesha mzigo wa uthibitisho kwa muathirika ziliishia kwa washambulizi wake kuachiliwa huru.
Kainat na familia yake, ambao sasa wanaishi kwenye nyumba chakavu ya vyumba viwili mjini Karachi, wanasema 'wamepoteza kila kitu', zimesema ripoti.
Filamu hiyo fupi, inayoitwa 'Outlawed in Pakistan', inaelezea simulizi ya mapambano ya kisheria ya Kainat dhidi ya wabaya wake. Filamu hiyo, kwanza ilifichuliwa katika Tamasha la Filamu la Sundance mwaka 2013, ilirushwa hewani kwa mara ya kwanza kwenye televisheni ya Marekani wiki iliyopita.
"Waliniambia mimi sio mwanaume kamili," kaka yake Kainat, Sabir, aliwaeleza watengenezaji filamu Habiba Nosheen na Hilke Schellmann.
"Kwamba umeshindwa kufuata utamaduni wako, umeshindwa kumuua dada yako."
Watazamani walitazama wakati Kainat alipokodisha wakili, kufanya mahojiano kwenye televisheni na kukata rufani dhidi ya maamuzi ya mahakama.
Lakini licha ya uwepo wake, msimuliaji wa filamu hiyo anaelezea jinsi jaji huyo alivyochambua madai yake kama 'matokeo ya burudani yake binafsi'.
Kufuatia kuachiwa kwao, wanaume hao aliowatuhumu wanashangaa kwanini alishindwa kubaki tu nyumbani 'na kunyamaza kimya'.
Filamu ya 'Outlawed in Pakistan' inamulika mwanga katika mapambano Kainat anayosisitiza hawezi kuachana nayo.