Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4652
↧

NDEGE YALAZIMIKA KUTUA KWA KUSOTA BAADA YA MABURUDUMU KUGOMA...

$
0
0
Ndege hiyo baada ya kutua.
Ndege ya US Airways ikiwa na abiria 34 ndani yake ililazimika kutua kwa kusota kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Newark baada ya kupata matatizo katika mfumo wa magurudumu yake juzi.

Abiria waliojawa hofu walifanikiwa kutoka kwenye ndege hiyo bila madhara baada ya rubani wa ndege hiyo - aliyetajwa na mashuhuda kama Edward Powers - kufanya kishujaa utuaji wa dharura.
Msemaji wa US Airways, Davien Anderson alieleza kwamba turboprop, ndege ya injini mbili ambayo iliruka Philadelphia muda mfupi kabla ya Saa 5 usiku wa Ijumaa ilitua salama Newark huku magurudumu yake yakiwa yamerudi ndani takribani Saa 7 alfajiri ya Jumamosi.
Anderson alisema ndege hiyo, iliyokuwa ikimilikiwa na Piedmont Airlines, ilikuwa imebeba abiria 31 na wafanyakazi watatu.
Anasema ndege hiyo ilizunguka uwanja wa Newark wakati wakihangaika kushusha magurudumu yake. Baada ya majaribio kadhaa kushindikana kuwezesha magurudumu kutoka nje, ndge hiyo ikatua kwa kusota kutumia tumbo lake.
Anderson anasema abiria hao waliondolewa uwanjani hapo kwa kutumia basi. Anasema US Airways inashirikiana na Bodi ya Taifa ya Usalama wa Usafiri ambayo inachunguza tukio hilo.
Picha za video za tukio hilo zinaonesha cheche zikilipuka kutoka chini ya ndege hiyo wakati ikisoka kwenye njia ya kutua/kuruka.
Kwa namna ya kushangaza hakuna moto ulioripotiwa baada ya kutua huko kwa ajabu lakini wafanyakazi waliokuwa ardhini walimwaga povu kwenye njia hiyo kwa tahadhari kama ungetokea moto.
Hakuna ripoti zozote za mvurugiko kwenye uwanja huo wa ndege ingawa njia moja ya kuruka/kutua ndege bado imefungwa wakati uchunguzi ukiendelea.
↧

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4652

Latest Images

Trending Articles