Baba mmoja alinunua roboti maalumu kwa lengo la kudhibiti tabia ya uongo katika familia yake. Ni kwamba mtu akisema tu uongo basi roboti linamtandika vibao dakika hiyo hiyo.
Siku moja baba akamuuliza mwanae: "Mage umekuwa wa ngapi kwenye mtihani?" Mtoto akajibu: "Wa kwanza!" Bila kuchelewa roboti likampiga kibao. Baba akaanza kujinadi: "Enzi zangu mimi kila mtihani nilikuwa nashika namba moja!" Saa hiyohiyo roboti likamnasa kibao. Mtoto alipoanza tu kucheka, mara mama akatokea na kumfokea: "Unacheka nini sasa, hujui kama huyo ni baba yako?" Bila kuchelewa roboti, likamtandika kibao na yule mama! Duh...↧