Quantcast
Channel: ziro99blog
Viewing all articles
Browse latest Browse all 4605

'JESHI MAALUMU' SASA KUKABILI UJANGILI WA WANYAMAPORI...

$
0
0
Mmoja wa tembo waliouawa na majangili.
Katika kukabiliana na ujangili kwa wanyamapori nchini, Serikali imeanza mchakato wa kuanzishwa kwa Mamlaka ya Wanyamapori Tanzania itakayokuwa mithili ya `jeshi maalumu’ la kulinda wanyama hao.

Imeelezwa kuwa mchakato huo unatarajiwa kukamilishwa na wabunge katika Bunge la Novemba mwaka huu kwa kupitishwa kwa sheria itakayoeleza adhabu zitakazoendana na thamani ya wanyama hao.
Katika kuhakikisha lengo hilo linafanikiwa, jana Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki alikutana na makatibu wakuu viongozi, mawaziri, makatibu wakuu, wakurugenzi na watendaji wengine waliopitia wizara hiyo kwa nia ya kupata michango yao ya kuanzisha mamlaka hiyo.
Akizungumza wakati wa kufungua kikao hicho cha wadau, Waziri Kagasheki alisema kuundwa kwa mamlaka hiyo kutabadili sheria ya wanyamapori kwa kuwa adhabu za wanaoua wanyamapori kwenda sambamba na thamani ya wanyama hao.
“Adhabu za wanaofanya ujangili kwa wanyama wetu ni za mzaha kwa kulipa fidia ndogo na vifungo visivyoendana na thamani ya wanyama, lakini katika sheria ya sasa tutakuwa na adhabu kali zenye kuendana na thamani yake,” alisema.
Alisema katika kuunda sheria  hiyo wanakusanya maoni ya wazee hao wenye hazina ya masuala ya wanyamapori na kwenda kwa watu wengine ili sheria hiyo iwe ya watu.
Alisema mamlaka hiyo itasaidia kusimamia kwa ukamilifu rasilimali hiyo ya wanyamapori na wengine nje ya wizara kwani serikali imechoka na ujangili wa wanyama kuibiwa na kuuawa.
Naye, Ofisa Mkuu wa Utekelezaji wa Mipango katika wizara hiyo, Chikambi Rumisha alisema kumekuwa na ongezeko la kasi la ujangili kwa wanyama hivyo kutishia uchumi wa nchi.
Alisema sasa wameamua kurekebisha mifumo ya kiutendaji ili kuwe na ufanisi ambapo mamlaka hiyo itahusika na utekelezaji huku wizara ikibaki na masuala ya sera na sheria.
Alisema chombo hicho kitakuwa na mfumo wa kijeshi wenye silaha, mbinu za medani, vifaa vya kisasa vya kutosha na rasilimali watu wa kutosha kukabiliana na ujangili huo.
Akizungumza kwa niaba ya washiriki hao, Katibu Mkuu Kiongozi mstaafu Philemoni Luhanjo alisema katika kuimarisha ulinzi katika sekta hiyo lazima kuwe na ulinzi, wataalamu wa kutosha na vifaa vya kisasa.
Pia kuwepo na ushirikishwaji wa wadau hasa wananchi au mashirika yasiyo ya kiserikali katika ulinzi, ikiwa ni pamoja na kuwa na urafiki katika eneo lenye wanyama hao kwa kutoa huduma za ziada katika vijiji hivyo kusaidia kulinda na kutoa taarifa.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 4605

Trending Articles