![]() |
Hali ilivyokuwa eneo la tukio mara baada ya kulipuka kwa bomu hilo. |
Hatima ya watuhumiwa 12 wa tukio la kurusha bomu katika Kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Olasiti mkoani Arusha, wanaoshikiliwa na Polisi inatarajiwa kujulikana leo.
Hayo yalisemwa jana na Kamanda wa Polisi jijini Arusha, Liberatus Sabas wakati akizungumza na mwandishi wa habari hii jana kwa njia ya simu.
"Kesho (leo) tutatoa mwendelezo wa taarifa ikiwemo kujua lini watafikishwa mahakamani kwa sasa siwezi kusema.’’
Awali mwishoni mwa wiki polisi walitangaza donge nono la Sh milioni 50 kwa mtu yeyote atakayefanikisha kufichua mtandao wa kigaidi nchini.