![]() |
Benedict XVI (kushoto) akisalimiana na Papa Francis I. |
Kuzorota kwa afya ya Papa Emeritus Benedict XVI kumemfanya kubakia nusu ya umbile lake la siku za nyuma, imedaiwa jana.
Kardinali wa Ujerumani ambaye alimtembelea Papa huyo alisema alishitushwa jinsi hali ya afya yake ilivyokuwa imezorota.
Joachim Meisner, Askofu wa Cologne, alimtembelea Benedict mnamo Machi 18, mwaka huu siku moja kabla ya Papa Francis kumrithi. Ilikuwa wakati huo Benedict akiishi huko Castel Gandolfo, makazi ya papa wakati wa kipindi cha majira ya joto yaliyoko nje ya mji wa Roma.
Alikuwa amestaafu kuyoka Kiti hicho cha Mtakatifu Petro mnamo Februari 28, mwaka huu.
Kardinali Meisner alilieleza Shirika la Habari la Kanisa Katoliki (KNA) alishitushwa na jinsi alivyokuwa amenyauka.
Alisema: "Alionekana kama amekuwa nusu ya umbile lake. Tangu mwanzo sikukubaliana na kujiuzulu kwake.
"Lakini nilipomwona mapendekezo yangu yakatoweka kabisa. Kiakili, hatahivyo, yuko madhubuti kabisa."
Rasmi, Papa huyo mwenye miaka 86 alijiuzulu sababu ya alichoelezea kama 'kuzorota kiuwezo, vyote mwili na kiroho'.
Kwa upande wake, taarifa yake binafsi ya kujiuzulu Papa Benedict ilizungumzia uwezo wake kuwa 'hauendani na uteshelevu katika taasisi hiyo ya Petrine.'
Paloma Gomez Borrero, mwandishi wa habari mzoefu huko Vatican kutoka Hispania, alisema kwamba katika siku 15 zilizopita papa huyo wa zamani amekuwa akipitia hali ya kuzorota afya yake ya kimwili.
Alisema: "Hatutaweza kuwanaye kwa muda mrefu zaidi", limeripoti gazeti la The Daily Telegraph, ingawa hili limeripotiwa kukanushwa na vyanzo vya habari vya Vatican kwamba limetiwa chumvi.
Ilielezwa kwamba Benedict amepatiwa ahueni kwa kutokuwa tena Papa.
Kaka yake alilieleza gazeti hilo kwamba bado anasumbuliwa na matatizo ya Kanisa hilo, lakini 'hakika amepata ahueni kutokubeba uzito huo wa Kanisa hilo katika mabega yake.'
Georg Ratzinger, mwenye miaka 88, ambaye ni padri, alisema mdogo wake hakuwa akisumbuliwa na maradhi fulani.